Friday, February 10, 2017

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT.ASHATU KIJAJI AZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘ECOBANK MOBILE APP’



Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili ya kurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipeana mkono na Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Bw. Peter Machunde mara baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia (katikati) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank-Afrika Bw. Ade Ayeyemi na Mkurugezi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei-Safo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch-Osei Safo akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Ecobank Mobile App’ ambayo ilizinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili ya kurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ecobank wakifuatilia kwa makini hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili yakurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Tanzania Bw. Peter Machunde akiteta jambo na Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa rasmi jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akipakata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania kuhusiana huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye programu ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Tanzania Bw. Peter Machunde.Mkuu wa kitengo cha huduma za kidijitali za kibenki Bw. Nachona Hussein akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Ecobank  Mobile App’ uliofanyika jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili ya kurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.


Ecobank Tanzania (ETZ) imezindua huduma mpya ya Ecobank Mobile App, hii ni njia rahisi na ya haraka ya kibenki kupitia simu za mkononi. Ecobank Mobile App itawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ikiwemo kuhamisha fedha - kote baina ya matawi na baina ya benki, kununua muda wa maongezi, Malipo ya Ankara, kuangalia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni, maombi na kuangalia taarifa za benki, Malipo ya kibiashara, pamoja na huduma za Kadi na hundi.

Zaidi, Ecobank Mobile App itawawezesha wateja wa benki kuweza kuzifikia akaunti zao kupitia simu za mkononi na chaneli USSD, hivyo kuwahakikishia unafuu, upatikanaji, na kasi kwa saa 24 kwa juma huku ikiwaondolea ulazima wa kwenda au kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo ambayo kwa sasa yapo nane (8).

Tukio hilo kwa sehemu kubwa lilihudhuriwa na halaiki ya watu ikiwa ni pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Ecobank, Wateja na Wafanyakazi wa benki, Watendaji wa Kampuni ya Ecobank, Wanafunzi, Wanadiplomasia, Viongozi wa Serikali, Wawakilishi kutoka Benki Kuu na washirika wa kibiashara wa benki hiyo.

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alikuwa Mgeni Rasmi katika tukio hilo. Aliishukuru ETZ kwa ubunifu huo ambao, alisema utaenda mbali sana katika kuharakisha na kuimarisha juhudi za ushirikishwaji kifedha nchini Tanzania.

Aliipongeza benki hiyo kwa kuunga mkono juhudi na kauli mbiu ya awamu ya tano ya “Hapa kazi tu” kutokana na kuzindua bidhaa ambazo zimelenga kuwarahisishia maisha watanzania.

“Badala ya watu kubeba fedha mkononi sasa watabeba kidigitali” alisema na kuongeza kuwa utaratibu huu sio salama tu bali ni rafiki kwa kuokoa muda hasa katika kipindi hiki cha “Hapa kazi tu”.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi katika kuhakikisha benki zinafanya kazi kwa usalama na kuunga mkono uchumi wa kutembea bila fedha taslim.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ecobank Bw. Ade Ayeyemi, idadi ya watu ya kuvutia na sifa nyingine za pekee nchini Tanzania zinaenea vema katika dira ya kampuni ya kuongoza ushirikishwaji wa kifedha barani Afrika. 
 
"Ecobank Mobile Appinawafungulia fursa kubwa wateja kwa kuwawezesha kununua, kufanya miamala na kufanya biashara bila kubeba fedha taslimu. Ni huduma unganishi ya aina yake na ya kwanza kuwahi kutolewa na taasisi yoyote na kutumiwa kwa pamoja katika nchi 33 za Afrika. Tunataka kuinua uwezo wa kidijitali kwa kuuweka kiuhalisia uwezo huo katika vidole vya viganja vyenu." Alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa ETZ, Bw. Enoch Osei-SAFO alisema: "Siku ya leo ni ishara ya kilele cha safari yetu ya kuiweka mahali pazuri ETZ kama lango la kidijiti la kuvutia nchini Tanzania kwa watu binafsi, wafanyabiashara, wachuuzi na taasisi za serikali. 
 
Ecobank Mobile App pamoja na mambo mengine, itawasaidia wateja wetu kununua na kulipa bila kutumia fedha taslimu tena kwa urahisi zaidi kuliko walivyowahi kufikiri". Mbali na huduma zake za kibenki za kwenye mtandao kwa watu binafsi na wafanyabiashara pamoja na Ecobank Mobile App na visa/MasterCard za benki, “msukumo wa kidijiti” wa ETZ utashuhudia benki hii ikisonga mbele katika ufumbuzi zaidi wa ubunifu wa kidijitali ikiwa ni pamoja na kadi Prepaid, Akaunti ya Ecobank Xpress na Masterpass QR katika miezi ijayo mara tu vikwazo vyote vya udhibiti vitakapokuwa vimeondolewa. Ecobank Mobile App ilizinduliwa kwa mara ya kwanza huko Lagos, Nigeria, tarehe 20 Oktoba, 2016.

Katika kipindi kifupi kijacho, wateja wa ETZ watakuwa pia na uwezo wa kutumia Ecobank Mobile App kufungua akaunti ya Ecobank Xpress, ambayo ni akaunti rahisi ya kidijitali inayotamba kwenye e-KYC. Ecobank pia ni benki ya kwanza barani Afrika kushirikiana na Mastercard, huduma inayoongoza katika malipo ya kimataifa na teknolojia, kuleta wateja wake Masterpass QR.
 

Ufumbuzi huu mpya, usiotumia fedha taslimu katika kufanya malipo, utawezesha kuhifadhi kwenye mtandao na katika kupitia simu ya mkononi. Tunaishukuru Ecobank, kwani wafanyabiashara nchini Tanzania katika siku za usoni watakuwa na uwezo wa kutumia huduma ya Masterpass QR kukuza biashara zao.

No comments: