Friday, February 10, 2017

DC KOROGWE AWAONYA WATUMISHI WA HALMASHAURI KUACHA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha Azidu Kaonekana wa pili kulia ambao wameshirikiana na A Better World kutoka Canada kufanya ujenzi wa majengo matatu ya maabara kwenye shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayan
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Martha Kusare kulia akipokea msaada wa sola ya mobisol  kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema ili kuweza kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi yao ambapo sola hiyo na ujenzi wa maabara tatu zilizojengwa na taasisi hiyo  iligharimu kiasi cha sh.milioni 75
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka akifuatilia maendeleo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wilayani korogwe Mkoani Tanga
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Patema Jerome Massawe wakati wakitembelea maabara hiyo
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka wa pili kulia akiangalia namna wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wanayofundishwa masomo ya sayansi mara baada ya kukamilika maabara hiyo
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Patema,Jerome Massawe
 Muonekano wa Majengo ya  maabara hizo



WATUMISHI katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameonywa kuacha kutumia vibaya fedha za miradi zinazotokana na wafadhili kwenye maeneo yao kwani watakaobainika kufanya hivyo watashughulikiwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hayo yalisemwa  na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert  Gabriel wakati akipokea taarifa ya umalizaji wa majengo ya matatu ya maabara yalijengwa na taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayani humo.

Aidha wao kama viongozi wa serikali wilayani humo hawatakuwa na mdhara  na watumishi ambao watabainika kuihujumu miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao na wafadhili mbalimbali kwani kufanya hivyo kunachangia kurudisha nyuma kasi ya ukuaji wa maendeleo.

“Nisema wazi kuwa watumishi badilikeni kwani mimi kama kiongozi wa  wilaya hii sitamfumbia macho mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo kwenye wilaya hii na niwaonye wenye tabia kama hiyo waiache mara moja.

Aidha alisema lazima watu wabadilike hasa wale wanaopewa majukumu ya  kusimamia miradi hiyo kutoka kwa wafadhili na wawe wawazi wakati wa utekelezaji wake ili kujenga heshima kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

“Baadhi yetu tunatumia fursa hizo vibaya na kujinufaisha kupitia fedha  za wafadhili kinyume na hitaji husika,kufanya hivyo kunaweza kuwakimbiza wadau hao wa maendeleo na kutia doa kwa Taifa”Alisema Gabriel.

Awali akizungumza katika kikao hicho Afisa Elimu sekondari Halmashauri  ya Korogwe Vijijini Patricia Mbigili alisema pamoja na jitihada kubwa ambazo wanazifanya kuhakikisha wanakamilisha suala la maabara lakini mpaka sasa zilizokamilika ni 5 kati ya 78 katika shule 26,ambapo kunahitajika maabara 3 kwa kila shule ikiwa ni za chemia,physician na bioligia.

Alisema ili kukabiliana na tatizo la ufaulu wa masomo ya sayansi 
katika shule za sekondari maabara na uwepo wa walimu wa masomo hayo unahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kuwajengea uwezo wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Mbigili alisema jukumu la kuboresha miundombinu ya shule na makazi ya  walimu ni la wananchi wote,serkali na taasisi zinazojitolea ili kutimiza azma ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu kama ilivyoanza kwa madawati na elimu bure.

Naye kwa upende wake, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Azidu Kaoneka  alisema umaliziaji wa maabara 3,nyumba 1 ya walimu na kuwawekea kifaa cha kuzalisha umemekupitia jua (mobisol) ambapo kiasi cha shilingi milioni 75 zimetumika.

Azidu alisema taasisi hiyo inaimani kubwa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na serikali wanaweza kujenga mazingira rafiki ya walimu na wanafunzi kwa kuboresha miundombinu ya mashule pamoja na nyumba za walimu kama ilivyofanyika shuleni hapo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: