Saturday, February 18, 2017

MKURUGENZI MKUU ATCL AKAGUA UWANJA WA NDEGE WA SONGEA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge kushoto akimweleza jambo mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi ofisini kwake mjini Songea leo, ATCL kupitia ndege zake za Bombadier zitaanza safari zake kati ya D,slaam na Songea mkoani Ruvuma baada ya wiki sita.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi akiangalia chumba kimojawapo cha kupumzikia abiria katika uwanja wa ndege wa Songea ambapo shirika hilo kupitia ndege zake aina ya Bombadier linatarajia kuanza safari zake mkoani Ruvuma hivi karibuni,kulia ni meneja wa uwanja wa ndege wa Songea Fasha Valentin.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma Fasha Valentin akiumueleza jambo mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege ATCL mhandisi Ladslaus Matindi juu ya ukarabati unaoendelea ambao utatoa fursa kwandege za shirika hilo kuanza safari zake kati ya maeneo mengine ya Tanzania na Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni,kulia ni meneja wa ATCL mkoa wa Mtwara na Ruvuma Esther Mahiga.
Meneja wa mamlaka ya usalama na usafiri wa Anga mkoani Ruvuma Janeth Lwiva wa pili kulia akitoa maelezo juu ya usalama katika uwanja wa ndege wa Songea kwa mkurughenzi mkuu wa shirika la ndege ATCL Mhandsi Ladslaus Matindi alipoytembelea uwanja huo, kulia meneja wa uwanja huo Fasha Valentin, na wa pili kushoto meneja wa ATCL mkoa wa Mtwara na Ruvuma Esther Mahiga.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege nchini ATCL mhandisi Ladslaus Matindi akikagua eneo la kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Songea,kulia meneja wa mamlaka ya usalama na usafiri wa Anga mkoani Ruvuma Janeth Lwiva.
Meneja wa shirika la ndege ATCL mkoa wa Mtwara na Ruvuma Esther Mahiga kushoto akimuongoza mkurgenzi mkuu wa shirika hilo mhandisi Ladslaus Matindi kukagua uwanja wa ndege wa Songea kabla ya ndege za shirika hilo kuanza safari zake mkoani Ruvuma, wa pili kulia meneja wa mamlaka ya usalama na usafiri wa Anga mkoa wa Ruvuma Janeth Lwiva na kulia meneja wa uwanja wa ndege wa Songea Fasha Valentin.
Mkurugenzi mkuu wa ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi kulia akimsikiliza meneja wa mamlaka ya usalama na usafiri wa Anga mkoa wa Ruvuma Janeth Lwiva juu ya usalama katika uwanja wa ndege wa Songea.

No comments: