Saturday, February 18, 2017

MBUNGE JOSEPH MBILINYI A.K.A SUGU AUNGURUMA JIMBONI KWAKE MBEYA


Mbunge wa Mbeya Mjini Mh.Joseph Othman Mbilinyi "SUGU"  amefanya mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mwenge,Jijini Mbeya. Kwenye mkutano huo Sugu ametumia sehemu ya hotuba yake kuwashukuru wana Mbeya kwa kumchagua kuwa kiongozi wao kwa kura nyingi zaidi na kumfanya kuwa Mbunge, Sugu licha ya kuongea mambo kwa mapana kuhusu serikali ya Jpm kwa kuminya haki kwa vyama vya upinzani na kuzungumzia kero ya tabia ya viongozi baadhi kuingilia kazi za wabunge, amempongeza Rais kwa kuingilia suala la vita ya madawa ya kulevya akidai kuwa awali lilikuwa likifanywa kisiasa na sio kukomesha janga hilo. Amesema kupitia Uteuzi wa Kamishna wa kushughulikia madawa ya kulevya kumeleta mwangaza na yeye kama mbunge anamuunga mkono kwa hilo.

Alijibu swali la mwananchi Isaac Nkoma akiuliza kuhusu Mikakati ambayo Halmashauri ya Jiji na Ofisi yake kama Mbunge juu ya suala la Ajira kwa vijana wengi wanaozidi kuongezeka mitaani wakitokea vyuoni na mashule, Mh.Sugu amesema ,,,"Hilo jambo ni mtambuka sana na jitihada binafsi zinahitajika kwa vijana hao ili wakati serikali ikiendelea na michakato ya ajira basi vijana waache kubweteka na kuwasihi kutumia muda vizuri kujiongeza na kutumia vipaji walivyojaariwa kujipatia riziki zao"
Aidha,wakiongea kwa nyakati tofauti Mh. Joyce Mwalalika Diwani viti maalum, Raphael Mwaitege katibu wa CHADEMA wilaya,Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya Mh.Joseph Mwachembe China Wa China wamewaasa wana Mbeya kuungana pasipo uoga ku Kukijenga chama na kushirikiana katika shughuli za maendeleo.
Aidha,Mwenyekiti huyo amewaonya vijana wanaotumiwa kisiasa kuharibu Amani kwenye mikutano ya hadhara kwani hata kwenye mkutano huo Vurugu ilitokea na kusababisha tafrani iliyokuja kusuluhishwa kwa Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuufanya mkutano huo kuendelea na kumalizika salama.
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi akiwasili Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge kwa ajili ya Mkutano
 Baadhi ya Viongozi Wanawake wa Chadema katika picha ya pamoja wakati Mkutano ukiendelea
  Kijana aliyesadikika ni mfuasi wa chama kingine  akiwa kakunjwa na  kijana wa Chadema mwenye koti jeusi kwa kumtuhumu kijana huyo kupiga picha Uwanjani hapo
 Polisi wakiwa wamemkamata kijana aliyekuwa akimpiga kijana mwenzake kwa lengo la kunusuru ugomvi huo na kuleta utulivu mkutanoni hapo.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.
MAELEZO NA THOBIAS OMEGA

No comments: