Saturday, February 18, 2017

KWA MUONEKANO HUU BADO NI NIDHAMU MBOVU KWA WACHEZAJI HAWA

 Mchezaji wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Janvier Basela Bukungu akiwa amevalia mavazi ya kawaida tofauti na wachezaji wenzake walivyovaa.
Mchezaji wa Simba Mohamed Husein Tshabalala akiwa amevalia mavazi ya kawaida tofauti na wachezaji wenzake walivyovaa.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Nidhamu ya mchezaji sio tu uwnajani au mazoezini bali ni hata pale unapokuwa umejumuika na wachezaji wenzako kitimu lazima uoneshe utofauti baina ya mchezaji na mtu mwingine.

Tatizo hili si mara ya kwanza kujitokeza katika timu zetu za kitanzania lakini limeendelea kukua zaidi hadi kurithisha wachezaji wa kimataifa (proffessional players) na wao kuamua kuanza kuishi kama sisi.

Mchezaji unapokuwa upo chini ya timu, iwe mnaenda uwanjani, safarini au hata mkiwa kambini (camp) lazima wawe katika sare ya pamoja (uniform) na hili ni kutokana na kutaka iwe kama sababu ya kuwatofautisha na jamii nyingine inayowazunguka.

Mohamed Husein Tshabalala, mchezaji tegemeo wa klabu ya Simba ambaye ukienda kumuuliza atakwambia anataka kuwa Proffessional Player nje ya nchi, hapa ameonesha nidhamu mbovu kwa kutokujumuika na kuvaa sare sawa na wenzake, hivi kama kuna timu inamfuatilia ikiona mwenendo huu watamfikiria kuwa ni mchezaji mzuri lakini hana maadili ya kazi yake na pia hajitambui.

 Mchezaji wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Janvier Basela Bukungu umechezea timu kubwa Afrika TP Mazembe, Esperance ya Tunisia lakini bado ameweza kuingia kwenye mkumbo huo na kusahau maadili ya kazi yake na swali je alipokuwa TP Mazembe na Esperance alikuwa anafanya hivyo au kwakuwa timu zetu za Tanzania zinaraulika?

Nini maana ya kuvaa sare pale mnapokuwa pamoja, sababu kubwa ni kutaka kuwa moja ya kitambulisho mbele ya jamii kuwa kuna wachezaji wa Simba wamefika hapa au wapo hapa. Pili kunapokuja kutokea tatizo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kukusanywa kwa pamoja kwani watakuwa wamevaalia sare za aina moja lakini pale itakapotokea hujavaa sare watu hawataweza kukutambua wewe kama ni mchezaji wa Simba.

Mategemeo yangu ni kuona uongozi wa Klabu ya Simba ukikemea sana kitendo hiki kwani ukiachilia maadili ya kazi  ila wachezaji hawa wamedharau agizo la benchi la ufundi na timu kwa ujumla, yaani wanafanya wanmachokitaka na hawaulizwi.

No comments: