Monday, February 13, 2017

Barclays kuendelea kuwekeza nchini, yafungua tawi mjini Morogoro

 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la kisasa la benki hiyo katika jengo la Shirika la Nyumba (NHC), mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na kulia ni  Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
 Mkuu wa Mauzo wa Benki ya Barclays Tanzania, (kushoto), akieleza kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo katika tawi jipya Barclays la mjini Morogoro katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo juzi. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed, mjumbe wa bodi, Dk. Suleman Mohamed na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays, Simon Mponji .

 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo mjini Morogoro. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays, Abdi Mohamed na  Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
  Meneja Masoko wa Barclays, Joe Bendera (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya uzunduzi wa tawi hilo. 
  Wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tawi la Morogoro wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya viongozi wa benki hiyo mara baada ya hafla ya uzinduzi wa tawi hilo.
Moja ya burudani zilizokuwepo wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya Barclays mjini Morogoro juzi.

No comments: