Na Ofisa habari Mufindi
Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi imeendelea kustawi katika sekta ya elimu ambapo tathimini ya matokeo ya darasa la saba ya Halmshauri hiyo yanaonesha kupanda kutoka asilimia 80.39 mwaka
2015 hadi asilimia 84.90% mapema mwaka jana, ikiwa ni sawa na
ongezeko la asilimia 4.51.
Akisoma
taarifa wakati wa kikao cha thimini ambacho huwakutanisha wakuu wa shule zote
za msingi na maaofisa elimu kata, Ofisa elimu taaluma wa Halmshauri ya Wilaya
ya Mufindi MRIAMU NGALA amebainisha, kuwa tathimini ya ufaulu huo umejumuisha
shule 143, watahiniwa elfu 05 mianne 38 ambapo wavulana ni elfu 02 miatatu 84
na wasichana ni elfu 03 na 54 huku wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa
kuendelea na elimu ya Sekondari wakiwa ni elfu 4 miasita 17 sawa
na asilimia 84.9.
Akisoma
taarifa hiyo Bi. NGALA ameainisha masomo ambayo wanafunzi wamefanya vizuri
zaidi kuwa ni pamoja na somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake ni asilimia 90. 51, Sayansi 90.13, Maarifa 87.88, Hisabati 56.34
huku somo la Kingereza likishika nafasi ya tano kwa asilimia 27.20.
Aidha,
afisa elimu huyo mwenye dhamana ya taaluma, ametaja baadhi ya malengo ambayo
walijiwekea na ndiyo yaliyochangia kufikia mafanikio hayo kuwa ni pamoja na
kufaulisha kwa asilimia 95, ufuatiliaji wa utendaji kazi, uwepo wa kambi za
masomo, udhibiti wa utoro wa Wanafunzi na Waalimu, ukamilishaji wa mada kwa
wakati na uwepo wa mazoezi ya kujipima.
Idara
ya elimu msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeweka uratibu wa kufanya
tathimini ya kina kwa kila mwaka mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mitihani
ya darasa la saba ili kuangazia mafanikio ya ufaulu kwa kila shule, kubainisha
changamoto na kuziwekea mikakati ya kuzikabili huku tathimini hiyo ikienda
sanjari na kutunuku zawadi na vyeti kwa wakuu wa shule na maofisa elimu kata
walifaulisha wanafunzi wengi zaidi hivyo kupandisha wastani wa ufaulu wa
halmashauri.
No comments:
Post a Comment