Saturday, December 24, 2016

Yaliyojiri Katika Vituo Mbalimbali vya Televisheni

SIMU.tv:Kampuni ya Flamingi imetoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo mwenge jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/iprKLCTuZNo

SIMU.tv:Jamii imeaswa kuunga mkono juhudi za serikali za kukomboa uhuru wa wanawake katika kutafuta usawa wa kufanya kazi. https://youtu.be/OGaOfxVu1KQ

SIMU.tv:Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza imejipanga kuwa na madawati ya ziada ifikapo januari 15 mwakani ili kutekeleza agizo la rais . https://youtu.be/CdjmbfpftRk

SIMU.tv:Wazazi na wadau wa elimu nchini wametakiwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wanafunzi hawajihusishi na tabia za utumiaji wa madawa ya kulevya. https://youtu.be/-s_jJjqj3a0

SIMU.tv:Mabingwa wateteziwa ligi kuu Tanzania bara jana wamekwaa kisiki kwa timu ya African Lyon baada ya kukubali sare ya bao moja kwa moja. https://youtu.be/PxxOv1VQqkQ

SIMU.tv:Vinara wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Simba leo watashuka uwanjani kutafuta alama tatu dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/3hXWctNCQ2I

SIMU.tv:Msanii wa muziki wa bongo Flavor Abdul Nasibu maarufu kama Diamond Platnumz anatarajia kuburudisha mashabiki wa muziki mkoani Iringa siku ya Krismas: https://youtu.be/9Go76OCoFDU

SIMU.tv:Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi  ametangaza tarehe ya uchaguzi mdogo kwa jimbo la Dimani visiwani Zanzibar pamoja na kata 20 za Tanzania bara. https://youtu.be/T21268iF8Tw

SIMU.tv:Matatizo yanayoikabili jamii katika kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu yameanza kupata ufumbuzi baada ya serikali kuanza kuagiza vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu. https://youtu.be/hcrm3cRO3RQ

SIMU.tv:Chama cha mapinduzi CCM kimeanza kukamata mali za chama hicho na kuwaondoa watu waliokodi  majengo ya chama hicho bila kulipa . https://youtu.be/4lfu68C0nrw

SIMU.tv:Jeshi la polisi mkoani Morogoro limefanunua kuhusu vifo vya watu 2 vilivyotokea baada ya polisi kupiga risasi juu kwa ajili ya kuwatawanya wananchi kwenye ghasia. https://youtu.be/auP6u1QtskA

SIMU.tv:Jeshi la polisi mkoani Dar es Salaam linawashikilia watu 4 kutokana na wizi wa gari na kasha la kuhifadhia fedha katika ofisi za mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania TIRA. https://youtu.be/mYWTVQWXzes

No comments: