Saturday, December 24, 2016

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ziarani China

 Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE Bw. Li Yi akimueleza Balozi Seif nia ya Kampuni yake ya kutaka kuibadilisha Zanzibar kimajengo endapo itaendelea kupewa tenda za Ujenzi walipokutana Mjini Beijing China.
Balozi Seif akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE  inayojenga Jumba la Treni Darajani Bw. Li Yi katika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing Nchini China. Nyuma ya Bwana  ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed.

Na Othman Khamis Ame, OMPR
Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi  inayoshughulikia miradi ya Ujenzi wa Bandari  na Madaraja Makubwa ya China { CHEC}   iko tayari wakati wowote kuanzia sasa kusubiri kuanza kwa harakati za ujenzi wa Bandari ya Mizigo ya Mpiga Duri Mjini Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bwana Li Yi akiambatana na Timu ya wahandisi wa Kampuni hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  hapo Ofisini kwake  Mjini Beijing Nchini China.
Bwana Li Yi alisema Wataalamu na wahandisi wa Kampuni yake  wameshakamilisha taratibu zote za kufanya Utafiti wa ujenzi huo baada ya  kupewa nafasi hiyo kufuatia tenda iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Mradi huo.
Alieleza kwamba Kampuni hiyo kongwe Duniani iliyoasisiwa mwaka 1837 hivi sasa imebadilika kiutendaji  ndani ya kipindi cha miaka miwili  kwa kuzingatia zaidi sheria na taratibu wa Kimataifa kitendo chacho kimeleta mafanikio makubwa kwa  Kampuni kiasi cha kuweza kuaminiwa na Taasisi na Mataifa tofauti Duniani..
Bwana Li Yi alisema CHEC kwa sasa ina uwezo wa kuendesha miradi ya Uvuvi, huduma za Maji, majengo ya bishara kubwa  { MALL }pamoja na miundombinu ya miradi ya umeme na hata kilimo.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliufahamisha Uongozi wa Kampuni nhiyo ya CHEC  kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina pingamizi yoyote kwa uwamuzi wao huo wa kujihusisha na miradi mengine ya kiuchumi.
Balozi Seif  alisema chakuzingatia  zaidi katika miradi yao mipya  wanayotaka kuianzisha ni kuandika barua  za maombi na kuziwasilisha kwa Mamlaka inayohusika na Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} kwa hatua zinazofaa.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake  alifanya mazungumzo na Uongozi wa Kapuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya Mjini China chini ya Mwenyekiti wake wa Kanda ya Afrika Bwana Hu Bo.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton  Mjini Beijing Bwana Hu Bo alisema Kampuni ya CRJE imeamua kuibadilisha Zanzibar kimajengo mazuri yakiwa na hadhi ya kisasa inayokubalika Duniani endapo wataendelea kukabidhiwa  tenda za kazi hizo.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyekiri uwezo mkubwa iliyonayo Kampuni hiyo ya Ujenzi ya CRJE baadaye mchana alionana kwa mazungumzo na Uongozi wa  Kampuni Kubwa  inayoongoza Duniani katika uendeshaji wa  Miradi ya Umeme ya TBEA.
Balozi Seif  aliueleza Uongozi huo wa TBEA chini ya Makamu wa Rais wake Bwana Wang  Pinshan kwamba Wataalamu wa Taasisi hiyo wana fursa ya kuangalia namna  wanavyoweza kuisaidia Zanzibar katika huduma mbadala  ya nishati ya Umeme.

No comments: