Saturday, December 24, 2016

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA UJENZI WA MAKAZI YA ASKARI MAGEREZA JIJINI DAR, AMPONGEZA KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NAMNA ALIVYOJIPANGA KUSIMAMIA UJENZI

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb)  akisalimiana na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016(wa kwanza kushoto) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (Mb).
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akikagua Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kabla ya kukagua eneo la ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akipokea Salaam ya heshima kutoka Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kabla ya kukagua eneo la ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo ambazo zinatarajiwa kujengwa katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam unakamilika ipasavyo.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza  alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
 Baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).
 Meneja Ujenzi wa Mamlaka ya Majengo nchini – TBA, Arch. Humphrey Killo akitoa maelezo ya kitalaamu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua eneo la ujenzi wa nyumba hizo za makazi ya askari kama inavyoonekana katika picha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: