Saturday, December 24, 2016

KUELEKEA KRISMASI: BARAZA LA VIJANA CHADEMA ARUSHA MJINI WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA MKOA MT MERU KUOKOA WENYE UHITAJI

VIJANA kutoka Baraza la Vijana wa CHADEMA  (BAVICHA) Wilaya ya Arusha Mjini  wakiungwa mkonoba baadhiya wananchi wengine wamefanya zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia hospitali yaMt Meru inayokabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali inayochangia ongezeko la vifo hasa akina mama wakati wa kujifungua. 
Akizungumza  jana katika katika Hopsitali ya Mt Meru, mratibu wa zoezi hilo kwa upande wa wachagiaji, Katibu wa BAVICHA Wilaya ya Arusha Mjini ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Glory Kaaya alisema zoezi hilo limefanyika maalum kama tukio la kuaga mwaka huu wa 2016 kwa kuwahamsiaha vijana wenzake na wanajamii wengine kujitolea kuchangia na kusaidia kupunguza upungufu wa damu katika hospitali ya Mt Meruwakiamini mchango wao utasaidia kuokoa maisha ya watu wengi.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliojitokeza kuunga mkono zoezi hilo ni pamoja na Mbunge wa Simanjiro Mh James Olemiya, Naibu Meya Jiji la Arusha Viola Likindikoki pamoja na baadhi ya madiwani wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha akiwemo Ddiwani Ephata Nanyaro wa Kata ya Levolosi na Rick Moiro wa Kata ya Moshono
Wataalamu wa afya wa Hopsitali ya Mt Meru ya Jijini Arusha wakiwa katika maandalizi ya kufanikisha zoezi la kutoa damu kutoka kwa wachangiaji ambao walijitokeza jana kusaidia upungufu uliopo hospitalini hapo. Wengine pichani ni baadhi yaviongozi na wanachama wabaraza la vijana la CHADEMA wilaya ya Arusha Mjini waliojitokeza kuchangia damu kwa hiyari. 
Sehemu ya damu ambayo ilipatikana jana itakayowafaa wahitaji na kusaidia tatizo la upungufu wa damu

Mwenyekiti waBAVICHA Arusha Mjini ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Innocent J Kisanyage akijaza fomu maalumu kablaya kutolewa damuMtaalamu wa afya akiendelea nahuduma ya uchangiaji damu
Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Ephata Nanyaro akiendelea kutolewa damu
PICHA NAMAELEZO: ARUSHA255 BLOG

No comments: