Sunday, December 11, 2016

VIJANA WANAWEZA KULETA MAPINDUZI YA VIWANDA VINAVYOJENGWA –WAZIRI MPANGO

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema vijana ndiyo wanaweza kuleta mapinduzi ya sekta ya viwanda vinavyojengwa. 

Dk.Mpango ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ameseama vijana lazima wachangamkie fursa ya viwanda pamoja na ujasiriamali. 

Amesema nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaohitaji hivyo sekta binafsi ndiyo inaajiri sehemu kubwa ikiwemo kujiajiri. Dk. Mpango amesema sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu ambao ni vijana wa kufanya hivyo kwa ujuzi wao. 

Aidha amesema kila mtu anatakiwakulipa kodi ili serikali iweze kutoa huduma kwa wananchi na kodi isipotumika kwa malengo wananchi wanaweza kuhoji kodi i yao.

Dk. Mpango amesema serikali haitaki kuibana sekta binafsi ishindwe kupumua kutokana na kodi kinachofanyika kuangalia uwezo wa ulipaji kodi kwa kilakinachozalishwa. Waziri huyo ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Chakula Dawa (TFDA), kuwatembelea wajasiriamali ili kuweza kupata changamoto zao. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari mara baada ya kutembelea maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda hilo katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akitoa maagizo kwa Meneja Uhusiano kwa Umma wa TFDA, Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda la TFDA katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakipata huduma katika banda la majani ya chai katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakipata huduma katika banda la Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam 
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

No comments: