Sunday, December 11, 2016

RUTAGERUKA:VIJANA NDIO WENYE KUBEBA UCHUMI WA VIWANDA


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Vijana wametakiwa kubeba uchumi wa viwanda wa Tanzania inayojengwa katika serikali ya awamu ya Tano ya Dk. John Pombe Magufuli.

Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka wakati wa semina ya vijana iliyofanyika katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.Amesema semina imefika muda mwafaka kutokana na nchi kwenda katika sekta ya viwanda ambapo vijana ndio sehemu yao.

Amesema sekta ya viwanda inategemea vijana ambao ndio waendeshaji wa viwanda katokana na ujuzi wao wa kuendea viwanda hivyo.Nae Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, amesema vijana wanatakiwa kutumia fursa ya viwanda pamoja na ujasirimali na kuachana na kufikiria suala la kuajiriwa.

Amesema Taasisi Doris Mollel Foundation,imeona inawajibu wa kutoa elimu kwa vijana katika kuendea sekta ya viwanda.Amesema kuwa kila mmoja akatumia nafasi yake vizuri Tanzania inaweza kuondoka ilipo sasa na kusogea sehemu nyingine katika uchumi wa viwanda .

Akifunga simina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel amesema hakuna tatizo la ajira kwa vijana kuajiriwa kinachofanya vijana na kukosa mafunzo ya kazi ambayo wanakwenda kufanya.Amesema kutokana na mafunzo hayo kupitia maonesho ya viwanda atafanya mafunzo vijana ambao wanakwenda kutumika katika viwanda wakiwa wanakitu kichwani.

Mollel amesema hakuna mtu anaweza akamuachia kijana kiwanda kwa elimu alioipata anatachotaka mwajiri ni kijana mwenye ujuzi wa kutumikia kiwanda chake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza katika ufunguzi wa semina ya vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Taasisi Doris Mollel Foundation, Erick Kajwahura akizungumza katika semina vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa I-Learn East Afrika Limited, Noelah Ntukamazina akizungumza katika semina kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel akifunga semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu vijana wakiwa semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

No comments: