Na Teresia
Mhagama
Vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini watafaidika na mafunzo yatakayotolewa
na kampuni ya Empower kutoka Korea yatakayohusu utengenezaji vifaa Umeme Jua
ambavyo vinatumika kuwasha taa na kuchaji simu huku gharama yake ikiwa ni nafuu.
Hayo yamebainika jijini Dar es Salaam wakati wa kikao baina ya
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-Young na watendaji wa kampuni ya
Empower, inayotengeza vifaa hivyo.
Watendaji wa kampuni hiyo
walifika na baadhi ya vifaa hivyo vya Umeme Jua ili kuionesha Wizara
namna vinavyofanya kazi.
Dkt. Hong Kyu Choi, kutoka kampuni ya Empower alisema kuwa wamepanga
kutoa mafunzo hayo sehemu mbalimbali nchini ili vijana hao waweze kujiajiri na
pia kuwezesha wananchi hasa wa vijijini kupata huduma ya umeme.
Alisema kuwa mafunzo hayo pia yatatolewa kwa walimu wa Sayansi
nchini ili nao waweze kuwafundisha wanafunzi kuhusu teknolojia na hivyo kuwa endelevu.
“ Vijana wa Tanzania wana uelewa mkubwa sana hivyo wanachohitaji ni
kupata fursa ya kupata mafunzo kama haya na nyenzo ili waweze kujiajiri na pia
kuweza kufundisha watu wengine, hii itawasaidia wao kujiajiri pia,” alisema
Dkt. Choi.
Kwa upande wake, Profesa Muhongo alisema kuwa vifaa hivyo ni muhimu
sana hasa katika sehemu ambazo hazijafikiwa na nishati ya umeme na kwamba suala
la kutoa mafunzo hayo kwa vijana ni muhimu kwani itawawezesha kupata uelewa wa
teknolojia inayotumika kutengeneza vifaa hivyo pamoja na kujiajiri.
“Napata simu nyingi sana Watu wakilia, Umeme, Umeme, hii teknolojia
ni nzuri na itawasaidia wananchi wetu kupata mwanga na pia kuchaji simu zao,
hivyo nawakaribisha kuanza kutoa mafunzo hayo mwezi Machi mwakani,” alisema Profesa
Muhongo.
Hii ni mara ya Pili kwa Profesa Muhongo kukutana na Watendaji wa
kampuni hiyo ambapo mara ya kwanza alikutana nao mwishoni mwa mwezi Novemba
mwaka huu ambapo Balozi wa Korea hapa nchini alifika kuitambulisha kwa Waziri
wa Nishati na Madini na pia kueleza shughuli za kampuni hiyo katika sehemu
mbalimbali duniani.
Katika Kikao hicho cha mwezi Novemba, Mtendaji wa Empower, Dkt. Choi alisema kuwa, kampuni hiyo imekuwa
ikitengeneza vifaa hivyo vya Umeme Jua kwa kutumia teknolojia ya kisasa tangu
mwaka 2011 na kwamba lengo lake ni kusambaza huduma hiyo vijijini ili
kuwasaidia vijana na wananchi kupata huduma ya umeme na kwa gharama nafuu.
Alitaja baadhi ya kazi ambazo wameshazitekeleza kuwa ni pamoja na
kubuni na kutengeneza Mfumo wa Umeme Jua katika Kituo cha ‘City Christian
Center (CCC)’ kilichopo Dar es Salaam pamoja na kutengeza Paneli za Umeme Jua
za gharama nafuu katika sehemu
mbalimbali Barani Afrika.

1 comment:
UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI
(Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)
MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA
kwa maelezo kamili piga namba +255 662978067
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
NAITWA DR, MDIRO piga 0662978067. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.
NIPIGIE 0662978067. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO
Post a Comment