Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imeshirikiana na UMOJA
SWITCH ATMS katika kuwawezesha wateja wake wa Airtel Money kufurahia
huduma za kifedha na kutoa pesa kwenye mashine za ATM za UMOJA SWITCH nchi
nzima bila kuwa na kadi ya ATM.
Ushirikiano huu mpya utasaidia
kurahisisha huduma za kifedha kwa watanzania na kuwawezesha kufanya shughuli
zao za kiuchumi na kijamii kwa ufanisi zaidi, wateja wa Airtel sasa wanaweza
kupata huduma za kifedha wakati wowote masaa 24 siku 7 za wiki kupitia mashine
za UMOJA SWITCH ATMs zilizoendea nchi nzima
ushirikiano huu pia
utasaidia katika kutanua wigo wa
mawakala wa Airtel Money ambapo wateja wa Airtel hawatakuwa na haja ya kufungua
akaunti ya benki wala kuwa na ya kadi ya ATM ili kupata huduma hii, kwa kupitia
mashine za UMOJA SWITCH ATMs mteja ataweza kufanya muamala kutoka kwenye simu
yake ya mkononi na maramoja kutoa pesa zake kwenye mashine ya ATM kwa gharama
nafuu. Kiwango kidogo kitatozwa kama tozo kulingana na kiasi cha pesa ambacho
mteja atatoa.
Akiongea wakati wa uzinduzi,
Meneja kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce alisema” kupitia huduma yetu ya
Airtel money tunaendelea kutumia technologia ya kisasa katika kuhakikisha
tunatoa huduma bora zinazotoa suluhusho na kutatua changamoto katika huduma za
kifedha kwa wateja wetu.
Ushirikiano huu kati ya Airtel na Umoja SWITCH utaleta
ufanisi na urahisi katika huduma zakifedha kupitia simu za mkononi”
Kupitia ushirikiano huu pia
tunaongeza idadi ya mawakala ambao kwasasa ni zaidi ya mawakala 85,000 nchini nzima,sasa
wateja wetu wanauhakika wakupata pesa kupitia mashine za ATM za Umoja SWITCH
wakati wowote.
Lengo letu ni kuhakikisha
tunaongeza idadi ya mawakala kwa kupitia njia mbalimbali na kuhakikisha huduma
za kifedha kupitia simu za mkononi zinapenya na kuwafikia watanzania wengi na
hivyo kuleta tija katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa ujumla.
Aliongeza Alphonce
Kwa upande wake Afisa
Mtendaji Mkuu wa Umojaswitch, Danford Mbillinyi alisema” kuingia
kwa makubaliano katika huduma ya Airtel Money kuthihirisha lengo letu la
kuchochea ushirikiano wamakapuni katika huduma za kifedha nchini.
Tumekuwa
ni sehemu ya Airtel katika huduma inayomuwezesha mteja kutoa pesa benki kwenda
Airtel Money na Airtel Money kwenda benki na sasa tunafungua milango mingine
kwa wateja wa Airtel Money kutoa pesa katika ATM zetu kwa urahisi na
uhakika kwa kutembelea katika ATM zetu nchi nzima.
Alisisitiza Umojaswitch iko tayari
kuungana na makampuni yanayoamini katika ushirikiano wa kibiashara kwani
tunatambua kwa kufanya hivyo kutaleta tija kwa wateja na uchumi wananchi”
Ili kupa huduma hii , mteja
atatakiwa kupiga *150*60# kupitia simu yake ya mkononi kisha kuchagua kutoa pesa kupitia ATM, kisha kuchagua UMOJA SWITCH ATM na kupata namba maalumu ya
kwaajili ya kutoa pesa. Namba
hiyo itatumika katika kutoa pesa kwenye mashine yoyote ya ATM ya UMOJA SWITCH
Tanzania. Kila token (namba) itakayotolewa itatumika mara moja na itadumu
kwa muda wa dakika tatu (3)
No comments:
Post a Comment