Friday, December 23, 2016

UHURU MUSIC YAKABIDHI ZAWADI ZA MILIONI 3 KWA KITUO CHA AMANI KIGAMBONI

 Mkurugenzi wa kituo cha Uhuru wa Music Centre, Maneno Sanga akikabidhi zawadi kwa mmoja wa watoto wa kituo cha Amani Kigamboni .
 Mkurugenzi wa kituo cha Uhuru wa Music Centre, Maneno Sanga akiwa na mkurugenzi wa Dege Stationary wakikabidhi zawadi wa watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu katika kituo cha Amani.
 Watoto wa kituo cha Amani wakibeba baadhi ya zawadi zilizoletwa na wadu hao.
 Mtoto Melvin Ndugulile akikabidhi vitabu kwa watoto wenzie wa kituo cha Amani kilichopo kigamboni.
 Mbunge wa Kigamboni ,Dk Faustine Ndugulile akibeba mzigo ambao amepeleka katika kituo hicho cha Amani




Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Kamapuni ya Uhuru Music centre kwa kushirikiana na Dege Stationary imetoa msaada wa vifaa vya shuleni na chakula vyenye thamani ya  kiasi cha fedha shilingi milioni 3 kwa ajili ya kituo cha watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Kigamboni.

Akizungumza na globu ya jamii mkurugenzi wa Uhuru Music Centre, Maneno Sanga amesema kuwa wameamua kutumia sikukuu hii kutoa zawadi kwa watoto ambao ni yatima hili nao waweze kupata maisha sawa kama watoto wengine waliopo majumbani wakiwa na wazazi wao wakati huu wa msimu wa sikukuu.

“katika zawadi hizi tumeweza kuleta vyakula ,vitabu pamoja na nguo za shule kwaajili ya watoto ambao wanataraji kujiunga na darasa la kwanza hapo mwakani hili mlezi wao asipate tabu ya kuingia gharama ya kuwanunulia vifaa” amesema Sanga.

Amesema kuwa alipowaza kutoa zawadi kwa watoto yatima alimpigia simu rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigamboni ,Dk Faustine Ndugulile ndipo alipoweza kumuunganisha na kituo hicho cha Amani.

Kwa upande wake mbunge wa Kigamboni Dk.Faustine Ndugulile, amesema kuwa anamshukuru sana bwana Sanga kwa msaada wake kwa kushirikiana na rafiki zake kwa kuona kama Kigamboni ni sehemu muhimu ya kutoa msaada huo.

Amesema kuwa vipo vituo vingi sana na Sanga ana marafiki lakini akaona Kigamboni ndio sehemu atayopeleka zawadi hiyo kwa watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na kuchagua kituo cha Amani kama sehemu mojawapo.

1 comment:

Anonymous said...

Very impressive job and it is great to download free ringtones for your phone.