Kwa mara nyingine tena EFM redio imegawa makapu ya sikukuu leo tarehe 23/12/2016 kwa wasikilizaji wake
ikiwa kama ishara ya kusheherekea kwa pamoja katika msimu huu wa sikukuu. Efm
redio hugawa makapu hayo katika msimu wa sikukuu ya Krismasi na Iddi kwa takribani
mwaka wa tatu sasa.
Mwaka huu EFM redio ikishirikiana na wadau wake Dstv
wamewakabidhi makapu kwa watu 24 baada ya kuibuka na ushindi kwa
kufanikiwa kujibu maswali yaliokuwa yakiulizwa katika vipindi vya redio
kuhusiana na maudhui ya redio pamoja na wadhamini hao.
Akiongea Mkurugenzi Mkuu wa EFM redio Francis Siza, “Tunapenda kuwathamini na kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa namna moja au nyingine kwani wao ndio mchango mkubwa sana kwetu hivyo zawadi hizi za makapu ni shukrani yetu kwao”.
Makapu ya sikukuu yakiwa yamesheheni mazagazaga kibao pamoja na kingamuzi cha DSTV
Makapu ya sikukuu yakiwa yamesheheni mazagazaga kibao pamoja na kingamuzi cha DSTV
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema, akipeana mkono na Muigizaji wa Tamthilia Irene Paul katika uzinduzi wa ugawaji wa makapu hayo, wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Efm redio Francis Ciza, Kutoka kulia ni Mboto Haji (Muigizaji) Pamoja na Meneja Masoko Dstv Bwana Alpha Mria.
Meneja Masoko Dstv Bw. Alpha Mria kutoka kushoto akimkabidhi mshindi wa kapu la sikukuu wengine katika picha ni waigizaji wa tamthiria za Dstv Haji Salum (mboto) na Irene paul pamoja na Swebe Santana Mtangazaji wa kipindi cha uhondo, efm redio
Washindi wakapu wa sikukuu wakifurahi kwa pamoja
Makapu ya sikukuu kwa wasikilizaji wa EFM
Zawadi kwa msikilizaji
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema akiwapongeza EFM na DSTV kwa hatua hii ya aina yake
Makapu ya sikukuu kwa wasikilizaji wa EFM
Mazagazaga kibao
Meneja Masoko Dstv Bw. Alpha Mria kutoka kushoto akimkabidhi mshindi wa kapu la sikukuu wengine katika picha ni waigizaji wa tamthiria za Dstv Haji Salum (mboto) na Irene paul pamoja na Swebe Santana Mtangazaji wa kipindi cha uhondo, EFM redio
1 comment:
Nivizur ila no: hamtaj natumeandaa majibu,toeni mikoa yote
Post a Comment