Friday, December 23, 2016

SUALA LA KUACHIANA VITI VYA KUGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI KWA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)BADO KIZUNGUMKUTI ARUSHA

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia akiwa na Viongozi wa CUF mkoa wa Arusha Mwenye shati la blue ni Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF)mkoa wa Arusha Zuberi Mwinyi baada ya mazungumzo ya ushirikiano wa ukawa Hotel ya Safari jijini Arusha picha na Maktaba

                                       
                                   
                                        Na Mahmoud Ahmad Arusha.

Suala la kuachiana viti vya kugombea udiwani,ubunge  kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)bado kizungumkuti katika Kata ya Mateves wilayani Arumeru  ambapo CUF na CHADEMA wasimamisha wagombea hali inayopelekea kugawa kura za wagombea hao wa Ukawa.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.

Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.

Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.

“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.

Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la kukijenga chama kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

Suala la mgawanyo wa maeneo ya kugombea limekuwa likivichanganya vyama hivi licha ya kuwepo makubaliano yaliofanywa na vingozi wa vyama vine hali inayoonekana kutokuwa na muafaka katika jambo hili, mfano majimbo ya segerea chadema na cuf walisimamisha wagombea na kujikuta wakiangukia pua katika jimbo hilo,hali inayoonyesha hakuna makubaliano katika hilo.

“tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi
Juhudi za wanahabari kuwatafuta viongozi wa CHADEMA mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa chama na Katibu wa Kanda ya kaskazini wa chama hicho Amani Golugwa ziligonga mwamba baada ya simu zao kutokupokelewa kila walipopigiwa bado juhudi zinaendelea kuwatafuta ili waweze kujibu madai hayo.

No comments: