Friday, December 23, 2016

MBUNGU NDUGULILE AOMBA WIZARA KUINGILIA KATI TOZO ZA DALADALA DARAJA KIGAMBONI

Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuangalia upya tozo za daladala zinazo pita katika daraja la kigamboni ili kuweza kutoa unafuu kwa wananchi waishio Kigamboni kama ilivyokua madhumuni ya kujengwa kwa daraja hilo.

Akizungmza na globu ya jamii Dk Ndugulile amesema kuwa wananchi wamekuwa watumwa kwa usafiri kwa miaka mingi huku wakitegemea daraja liwe mkombozi lakini sasa imekuwa kinyume kutokana na gharama za kupita kwa daladala katika daraja hilo.

“gari moja yaani daladala linatakiwa kulipa shilingi 5000 huku kwa kila trip kitu ambacho ni gharama kuliko biashara yenyewe ambayo ni huduma kwa wanachi hivyo kwa hesabu za haraka kama dereva atafanya trip 10 atatakiwa kulipa shilingi 50,000/- kitu hicho kinawawia vigumu kufanya kwa madereva wa daladala” amesema Dk Ndugulile.

Amesema kuwa amefanya jitiada za kila namna kwa kuzungumza na mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF ambo wao ndio wanaendesha daraja hilo kwa kuwaandikia barua rasmi  hili waweze kupunguza tozo hizo kwa ajili ya daladala lakini bado aoni dalili.

Ameongeza kuwa gharama za mkazi wa Kigamboni katika safari za mjini ni kubwa kuliko mtu yoyote licha ya kuwepo kwa miundombinu ya barabara na vivuko bado gharama za kifedha ni juu katika kutumia miundombinu hiyo.

No comments: