Tuesday, December 13, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM rais Dr John Pombe Magufuli leo amefungua na kuendesha mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho NEC. https://youtu.be/GlZA2MpY15U

SIMU.TV: Chama cha mapinduzi CCM kimefanya mabadiliko kadhaa ya kimfumo na kimuundo pamoja na kuteua wajumbe wapya kuziba nafasi za wajumbe walioteuliwa nyadhifa mbalimbali serikalini. https://youtu.be/2tC7TV0N7jY

SIMU.TV: Tanzania leo imezindua mpango kazi wa taifa wa miaka mitano unaolenga kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto ambapo utaanza kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018. https://youtu.be/q81BzICxbsw
  
SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa moja itakayoanzia Kurasini hadi bandari ya Dar es Salaam. https://youtu.be/yYQ1K5Ql-zA

SIMU.TV: Nchi zinazoendelea zimetakiwa kutafuta rasilimali zake za ndani ili ziweze kusaidizana na rasilimali kutoka nchi zilizoendelea ili kuwafikishia wananchi maendeleo. https://youtu.be/ACVr3UF1vg0

SIMU.TV: Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya wa taifa NHIF Anne Makinda, ametoa siku saba kwa msimamizi wa ujenzi wa jengo la mfuko huo mkoa wa Mbeya kutoa sababu za kutokamilika kwa jengo hilo. https://youtu.be/-wbjXfRQ_gY

SIMU.TV: Tatizo la ukosefu wa maji vijijini limetajwa kuwa chanzo cha magonjwa ya kipindupindu na kuhara ambapo pia vyoo vinavyotumiwa maeneo hayo vipo chini ya kiwango. https://youtu.be/l0puMtGPrq8

SIMU.TV: Serikali imesema kuwa itahakikisha ifikapo mwaka 2020 sekta ya viwanda itakuwa ikiongoza katika utoaji wa ajira kwa asilimia 40. https://youtu.be/7N0KQDheTcA

SIMU.TV: Mchango wa sekta binafsi katika kukuza sekta ya utalii umetajwa kuwa muhimu kutokana na kutoa huduma muhimu kwa watalii. https://youtu.be/awx56a3_9G0

SIMU.TV: Serikali ya India imeahidi kupanua wigo  wa biashara baina yake na Tanzania ili kuhakikisha nchi zote mbili zinapiga hatua ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi. https://youtu.be/fe7hL5AUVk8

SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limeanza mazungumzo na taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa ajili ya kushirikiana katika kutoa mafunzo kwa madaktari wa afya kwenye sekta ya michezo. https://youtu.be/mhTjJ-Tg1zY

SIMU.TV: Jumla ya waamuzi 18 wenye beji ya FIFA wameendelea na mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na shirikisho la soka TFF ili kuongeza ufanisi katika mashindao ya soka nchini. https://youtu.be/wgZgI7p4flM

SIMU.TV: Shirikisho la soka Tanzania TFF limevikumbusha vilabu vya soka vinavyoshiriki mashindano ya ligi kuu kuzingatia kanuni za mchezo huo ili kuepuka adhabu zasizo za lazima. https://youtu.be/exDwY7nXP5k

SIMU.TV: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imezindua kampeni ya Nogesha Upendo iliyolenga kuwanufaisha wateja wake msimu huu wa sikukuu. https://youtu.be/HAMI7n8XQv4

SIMU.TV: Klabu ya Leicester City imekamilisha hatua za awali za kumsajili mchezaji Wilfred Ndidi anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ikiwa ni njia ya kujiimarisha katika mzunguko wa pili. https://youtu.be/YSGXFAHQ-ww

SIMU.TV: Kikako cha halmashauri kuu ya CCM kimemalizika jijini Dar Es salaam na kufikia mabadiliko kadhaa ikiwemo kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya maamuzi; https://youtu.be/emtWGm-D9go

SIMU.TV: Chama cha wananchi CUF kimepitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama maandalizi ya chaguzi ndogo zitakazofanyika kujaza nafasi za madiwani na wabunge; https://youtu.be/FuCafC3HO68

SIMU.TV: Serikali imeahidi kuanzisha dawati maalumu katika shule za msingi na sekondari ili kuwalinda watoto wanaoshambuliwa na ukatili wa kijinsia; https://youtu.be/hrK8lbly4Rk

SIMU.TV: Baadhi ya wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wameiomba serikali wilayani humo kusaidia kuwarudisha wanaume waliokimbia familia zao; https://youtu.be/HL8-fd0vDCA

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Paul Makonda amesema umefika wakati wa kushirikiana na makampuni ya ujenzi nchini ili kuharakisha maendeleo; https://youtu.be/H3GDsKcmnJo

SIMU.TV: Wanafunzi 233 wanaosoma shule ya ufundi Mtwara hawana sehemu za kulala baada ya mabweni waliyokuwa wakiyatumia kuteketea kwa moto; https://youtu.be/TH2ua24pX4Y

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amebaini udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara wa mafuta ya kula baada ya kugundua mbinu wanazotumia kukwepa kodi; https://youtu.be/mBfwUtejIjk

SIMU.TV: Taasisi ya sekta binafsi nchini kwa kushirikiana na Trademark East Africa wamechapisha kitabu kinachoainisha taratibu za kuuza biadhaa nje ya nchi; https://youtu.be/UaOI2t5OhZw

SIMU.TV: Katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara amewataka wafanyabiashara na wawekezaji nchini kuzingatia haki za binadamu wanapotaka kuwekeza nchini; https://youtu.be/VnsfN0ZTpz8

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi na uchukuzi visiwani Zanzibar Balozi Alli Karume amesema kuanza kutua kwa ndege za shirika la ndege la Uturuki kutafungua mianya ya biashara visiwani humo; https://youtu.be/9mNYfTQanwg

SIMU.TV: Waamuzi wanaochezesha michezo ya ligi kuu Tanzania bara wameanza kupatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya kusaidia kuboresha maamuzi yao wakiwa uwanjani; https://youtu.be/mXEVx1EHBYs

SIMU.TV: Shirikisho la soka nchini TFF limevitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu kuhakikisha wanatunza kumbukumbu za wachezaji ili kuepusha migogoro baadae; https://youtu.be/T98YS7zAIsw

SIMU.TV: Wakuu wa vyuo vya Elimu nchini wametakiwa kuboresha viwanja vilivyopo katika vyuo vyao ili kusaidia kukuza sekta ya michezo; https://youtu.be/W_aYddCGxm0

SIMU.TV: Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amemshinda mshindani wake wa karibu Lionel Messi kwa kushinda tuzo yake ya nne ya Ballon D’Or; https://youtu.be/tA93rhlOvmQ


No comments: