Muheshimiwa Rais,
Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi na
shukran zangu za dhati kabisa, kwa muendelezo na juhudi zako ktk kuweka maslahi
ya nchi na wananchi mbele, moja ya juhudi hizo ni ktk harakati zako za usimamiaji
wa mapato ya umma na uboreshaji wa utendaji wa wafanyakazi wa mashirika na
taasisi za umma, ambapo sehemu moja ya juhudi hizo tumeziona ktk kupambana
kidhati ktk kukomesha ulaji rushwa makazini na kuondoa wafanyakazi hewa, hivyo
basi kuendeleza ufanisi ktk sekta za serikali na sekta ndogo ndogo za watu binafsi
kama mimi na wengine wengi tu, ambao wako ktk mkwamo mzima wa mzunguko wa hela
hapa nchini.
Hata hivyo muheshimiwa Rais, kuna
malalamiko ndani ya nchi na nje ya nchi hususan kwa wafanyabiashara wadogo
wadogo, yaani small na medium enterprise businesses, yaani mifano ya Matonya
Enterprises.
Kwanza kabisa, Muheshimiwa Rais, ningependa
kukufahamisha profile yangu in general, mimi ni mzawa na maskini ambaye anamudu
huduma zake za hapa na pale, nina nyumba mbili, moja ninaishi mwenyewe, na nina
duka dogo la kuuza spares za magari.
Nimeajiri wafanyakazi (Direct employment) wanne, na indirect
employement, ukiingiza na wafanyakazi wa part time, ninaweza kuwakisia kufikia
10, ukiingiza Mafundi, Madalali, nk.
Ninafanya kazi muda wa masaa 14-16 kwa siku, na mapumziko madogo siku ya
Jumapili. Yaani ninaweza kusema nina jitahidi sana ktk kazi yangu.
Sehemu kubwa ya kazi ambayo inanipatia
riziki yangu zaidi ya kuuza spares, ni uingizaji wa magari aina ya malori
kutoka Europe(UK, Sweden, Japan, nk) kuleta Tanzania, na vile vile ninaweza
kusema na kujiproud kuwa ni mlipaji kodi mzuri tu, ambapo malipo yangu ya kodi ni
wastani wa takribani Millioni za Kitanzania zisizopungua 180-200 kwa mwaka,
kupitia shirika la ukusanyaji kodi la TRA, Customs na ulipaji wa TBS(Vehicle
Inspections), lakini hata hivyo Muheshimiwa Rais kuna kitu kinanishughulisha
kimawazo na imenifanya niwe na maswali mengi bila majibu ya kuridhisha.
Kabla ya kuuliza hayo maswali yangu, kwanza
kabisa nataka nikupe hesabu ndogo kuhusiana na ulipaji kodi ambao ninaufanya
ktk sekta yangu ya kibiashara kwa kuweka wazi vikokotoo vya gharama za Kodi ya
importation ya unit moja tu ya Lorry kama ifuatavyo :-
Mathalani, Nikiagiza Gari Tanzania aina
ya Scania 94D, 6 * 2 ya mwaka 2001(lorry la kubebea mizigo kwenda mikoani) toka
dealership ya UK au Sweden.
Tathmimi ya malipo yapo ktk pesa ya
kigeni, US$
Import Duty $3848.63
Excise Duty $5773.00
VAT $4605.37
Customs Processing Fee $92.37
Railway Dev. Levy $230.92
Total Taxes $14550.29
Yaani Malipo yote yanaoingia serikalini ni 31,983,047.03
Tshs, Takribani milioni 32 pesa za kitanzania. Na hapo hapo Muheshimiwa
Rais sijaingiza gharama za Agent Fees, TBS certification ambazo ni £150, na
gharama nyengine ndogo ndogo.
Muheshimiwa Rais, Gari hio hio ninategemea
ikae sokoni, kwa muda wa takribani ya wastani ya miezi 3 mpaka mwaka 1, kwa
mustakbali wa hali ya mzunguko wa pesa ulivyokua mdogo kwa hivi sasa, sehemu
kubwa ya wateja wangu ni matonya kama mimi, ambao wanategemea mikopo ya bank,
retirement funds, ili kujiingiza katika shughuli na sekta ya usafirishaji na
wao wapate ugali wao.
Muheshimiwa Rais Hali ngumu sana ya
kimaisha, biashara yangu imeathirika na kushuka kwa mauzo ya 50% kwa mwaka huu
peke yake, hivi sasa binafsi niko ktk stage ya kuanza kula mtaji wangu, na
hivyo kuvunjika kimapato na kushuka kwa ulipaji kodi toka kwangu kuingia
serikalini, na hivyo basi hatma yake ni kufa kwa biashara, lakini mimi binafsi
na wengine, tunategemea hali itakua nzuri, panapo majaaliwa, Bank zitaanza
kukokepesha tena, sector ya usafirishaji binafsi kuanza kukua itakapofika kati
kati ya mwaka 2017, tukitegemea makubaliano uliyoingia nayo na nchi ya Congo,
na Rwanda hivi karibuni, kuweza kutumia bandari ya Dar.
Baada ya maelezo mafupi ya nini
ninafanya kupata riziki yangu, Hoja yangu Muheshimiwa Rais ni kama ifuatavyo!
Nimeona picha za magari za Dangote, kwenye
meli ambayo hivi karibuni imetia nanga na kushusha baadhi ya sehemu ya magari
600 siku mbili tu, baada ya kutoa ahadi aliyoitamka Dangote hapo ikulu
hii majuzi. Je hii ni calculated move, kukuhadaa wewe na kupata Baraka zako
Muheshimiwa Rais kwa upande wa Dangote, ukizingatia kuwa kauli zilizokua
zikitolewa na mawaziri husika zilikua ziko tofauti na matamko na steps
zilizochukuliwa na Dangote Cement, Mtwara, ie Kufunga Kiwanda kwa muda, nk. Kwa
hio alikua anategemea a better deal toka kwako, na kupata Baraka za kuingiza
magari chakavu, ndani ya nchi, na vile vile kuzitupilia mbali taratibu za
uingizaji wa bidhaa kama magari, kuhakikiwa ubora wake, yaani kupitia TBS, kama
ambavyo Matonya Enterprise tunazifuata.
Muheshiwa Rais, kwa kuangalia kwa ukaribu
vile vile Magari yaliyoshushwa sio magari mapya, Je TBS walihusishwa katika
uhakiki wa ubora wa magari hayo.
Muheshimiwa Rais Suala la pili ambalo
ndio muhimu katika yote, Je Dangote Group,
amelipia ushuru kiasi gani wa hizo gari,
au pia alipata Baraka za kuingiza hizi gari kwa ushuru mdogo bila ya uhakiki wa
TRA ?
Muheshimiwa Rais, kama nikikokotoa hesabu
za ushuru wa kila Lori, mathalani ushuru wa lori moja takribani ni US$10,000
ulinganisha na Scania ambapo hapo juu ni US$14550, kwa hiyo nimefanya mapungufu
ya zaidi ya US $4550, kama malori yote 600 yatalipiwa ni sawa US $ 6,000,000 sawa na rate ya leo ya
wastani wa 2200 per US $ 1, kwa hiyo Jumla ya kodi anayotakiwa kulipa Dangote
Group kwa uingizaji ya magari hayo ni Bilioni
13.2 TZShs, Je hizi pesa zimelipwa, kama tunavyolipa cash sisi Matonya
Enterprise, Je TBS imelipwa kama
inavyostahiki, takribani £150 *600 = UK £90,000 ni Milioni 252 Tzshs,
Ningependa sana Muheshimiwa Rais na taasisi
husika kutujibu maswali yetu hapo juu na kupatia vielelezo vya taratibu nzima,
zilizoihusisha idara zote, katika uingizaji wa magari 600, ie TBS, TRA, TPA na
Customs Office.
Na Suala la mwisho, Muheshimiwa Rais, Kuhusiana
na Dili la kununua Gesi moja kwa moja kutoka kwenye shirika la uzalishaji Gesi
kwa bei ndogo kabisa, Je mashirika mengine ya Matonya Enterprises, Cements
Companies, pamoja na mashirika makubwa ya binafsi kama Azam na mengineyo,
wataruhusiwa kupewa Gesi ktk bei hiyo hiyo aliyopatiwa Dangote na kukata
dearliship ya mtu wa kati ?,
Malalamiko yetu, Muheshimiwa Rais sisi wafanyabiashara wadogo wadogo, tumekua
tukisumbuliwa mara kwa mara na TRA, kuhakiki ulipaji wa kodi, ukizingatia
kwamba, malipo yetu yako wazi kupitia bidhaa tunazoziingiza through customs,
kodi hizi ambazo zinaongezeka mara kwa mara bila ya kutolewa proper notice,
mathalani kodi ya kuingiza lori aina ya Scania 94D, mwaka jana peke yake
imeongezeka zaidi ya mara moja, Muheshimiwa rais kodi tunazolipa si bidhaa
ndogo ndogo ni kodi ambazo haziwezi kufichika, na vile vile tunafanya malipo ya
VAT na filling ya Income Tax ya kila mwaka.
Muheshimiwa Rais, Naomba uzingatie kwamba,
wateja wetu ni wafanyabiashara wadogo wadogo, haya maongezeko ya kodi,
yanaathiri biashara zao, na yanaathiri ujumla wa ulipaji wa kodi kutoka sehemu
kubwa ya wafanyabiashara wadogo wadogo ambao ndio msingi wa uendelezaji wa nchi
kupitia malipo ya kodi, yanayofanyika mara kwa mara.
Kumbuka kwamba mimi Matonya Enterprise
tunalipa kodi kubwa in average ya Milioni 180-200 pesa za kitanzania kwa mwaka.
Mwisho kabisa, napenda kukushukuru
Muheshimiwa Rais kuisoma barua hii,
Mungu ibariki Tanzania na watu wake!
Hapa Kazi tu!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Andrew M!
No comments:
Post a Comment