Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile
(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota na tajiri duniani,
Floyd Mayweather Jr wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za
Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota
na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na promota nyota dunaini, Don King wakati
wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC)
unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota
na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota Wladimir Klitschko wakati
wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC)
unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota
na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa mkuu wa
54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi
wa Hollywood Marekani.
Promota
na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wa bondia nyota marehemu Mohammed
Ali wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani
(WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota
na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota mtaafu, Evander Holyfied
wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC)
unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Meneja
wa mabondia nyota nchini, Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile
amesema amejifunza na anaendelea kujifunza masuala mbalimbali ya
kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa duniani kupitia kwa mapromota
wakubwa kama Don King.
Ndambile
kwa sasa yopo nchini Marekani akihudhuria mkutano wa 54 wa Baraza la
Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) ulioanza jana kwenye ukumbi maalrufu wa
Hollywood. Akiwa Mtanzania pekee katika mkutano huo, Ndambile alisema
kuwa ameweza kujiunganusha na mapromota nyota duniani ili kuleta
maendeleo katika mchezo huo hapa nchini.
Alisema
kuwa ameweza kujadiliana na mapromota kadhaa ambao wanajua umuhimu wa
mchezo wa ngumi za kulipwa na kupitia kampuni yake ya Advanced Security
Limited ataweza kuandaa mapambano ya ngumi ya Kimataifa, yenye ubora wa
hali ya juu.
“Ubora
huo utatokana na mbinu za kutafuta masoko ya ‘kuuza’ pambano au
mapambano ya ngumi, mchezo wa ngumi unapendwa sana, hivyo nikiwa
Mtanzania pekee niliyepata fursa hiyo, nitaitumia ipasavyo ili kufikia
malengo niliyojiwekea na kwa faida ya Tanzania,” alisema Ndambile kwa
njia ya simu.
Alisema
kuwa ameweza kupata ‘contact’ za mabondia makubwa, lengo kuu ni
kuongeza wigo wa kazi zake na kufikia hatua ya juu kabisa katika ngumi
za kulipwa.“Kinchotakiwa
hapa ni kuwa makini na ‘serious’ katika kazi, ukichukulia mchezo wa
ngumi kimchez mchezo, hautafikia mbali, lakini ukiuchukulia kama kazi na
lengo ni kuendeleza vipaji na kujiongezea kipato, utafaidika wewe na
mabondia wao,” alisema.
Mbali
ya Dong King, Ndambile alikutana uso kwa uso na mabondia nyota kama
Floyd Mayweather, Amir Khan, Wladimir Klitschko, Evander Holyfield,
Lennox Lewis, Mike Tyson, Amir Khan na wengine wengi.
Alisema
kuwa umoja ni selaha pekee ya kuendeleza mchezo wa ngumi hapa nchini.
“Tofauti na wenzetu, hapa kwetu ni chuki, unafiki na mizengwe kibao,
wenzetu wanashirikiana, lengo ni ‘kuuza’ mchezo na si vinginevyo, mtu
akiandaa pambano, wanashirikiana wote,” alisema.
Mkutano
huo umeshirikisha wadau wa ngumi za kulipwa zaidi ya 1000, unatarajia
kumalizika Desemba 17. Mbali ya kutoa tuzo kwa mabondia na majadiliano
kadhaa, mkutano huo pia ulimuenzi bondia nyota, marehemu, Mohamed Ali
ambapo wadau wote walipiga picha kwenye sanamu yake.
No comments:
Post a Comment