KINANA AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA CCM, UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghtDu_5yb7gY-kSTvTt3SaiSyDfott_Fe5BlwDuWVKq37_Obzh0r5HvhHUw4ipy10cSemHVciewhWYRp_eWwU8TAxZWU8kgJyTCub3Cy_Nr3xDQPASw05ixlgh1Qe1tDIQhjADSQY55O8/s640/OTH_8106.jpg)
Jengo
la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga
jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa maelezo ya
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.
"Mpangaji
anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja
na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV
anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la
Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama
Zakia Megji na Mama Anna Abdallah.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi
jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama
Zakia Meghji.
Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji akizungumza wakati wa
uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini
Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa
la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM, Mama Anna Abdallah,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la
CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kuzindua
jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia baadhi ya wanachama
wa CCM wakati akienda kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo
Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Meghji
Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana akienda kukagua ndani ya jengo
Kinana akitazama ukumbi wa mikutano katika jengo hilo
Kinana akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM wakati akikagua jengo.
Samani ndani ya jengo
🔻
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi49cszV_2_yGowBzJ75a0Qnb38ha2oTF8FxhWuqx_8kDQP1ecl4uaX4sfOawCV5XNiyIp6UCeAeHgyTiEu5BOCzjWTXC92MfZ7PZ5YpQ30d4PAOb7so9jcEGaxLBfm_zBTn_KGYnvVIZWY/s640/BN640534.jpg)
jikoni
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBNXE4GAfpMz4Iebvsg7KQjXwTOViL5rX3iHy0yuP_O_8e-XSp8R0CbaABUm6NVRhS_maiAuJXGMZ7Rd9zpchyIV5C7pwuC3a4ROuq036tMx_mSH3TBHNm_lHNen53mYKi6vHXfn59Tq-n/s640/BN640543.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgiHUzOKc3EFOa1K4nXFT4CM9_hYYPjGE2_sYXJZCXrTLMCopuHg-THM4UagJvz0IzPAtLUeZ1TMaPxrcgl6Cul0MFBk6yzbXD6Mf2SpQaZdmrUAin2oC4v49evA55SCPT3Ncu23f9NpBv4/s640/BN640545.jpg)
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya viongozi kabla ya
kuondoka baada ya kuzindua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM, Upanga
jijini Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment