Ibada ya Krismasi Kitaifa imefanyika katika kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba huku viongozi wa dini wakitoa wito wa kudumishwa kwa amani na kuepuka vitendo vyovyote vya ubaguzi vinavyoweza kuwatenga wananchi.
Katika mahubiri hayo Askofu wa Dayosisi ya Ksikazini Magharibi Dokta Abednego Keshomshahara pia aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii badala ya kutegemea mafanikio yanayotokana na miujiza badala ya kufanya kazi.
Ibada hiyo ilianza kwa maandamano yaliyoongozwa na Askofu huyo ambapo Jumuiya ya Kikristo Nchini iliwakilishwa na Moses Matonya aliyetoa wito wa kuendelea kudumisha amani na kusisitiza upendo miongoni mwa wananchi
No comments:
Post a Comment