Wednesday, December 21, 2016

BODABODA ACHENI KUJIINGIZA KATIKA VITENDO VYA UHALIFU

ZAIDI ya wandesha bodaboda 500 wameweza kusajiliwa na mfuko wa Jamii wa GEPF katika fao la ‘Jikwamue Scheme’ ambapo huko wanapata huduma mbalimbali ikiwemo mkopo na siku za karibuni wataweza kufaidika na huduma za afya.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam na Ofisa Masoko, Elivine Faini, wakati wa kufunga mafunzo ya waendesha boda Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa yakifanyika katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ambapo GEPF walikuwa mmoja wa watoa mada.

Faini alisema wameamua kujikita kwa kundi hilo kutokana na ukweli kwamba hakuna mfuko ambao mpaka sasa umewafikia na kuongeza kwamba nao wana mahitaji kama ilivyo kwa watu wa sekta nyingine katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alisema ili kuweza kufaidika na fao hilo, mwendesha boda anatakiwa anatakiwa achangie sio chini ya miezi sita, ambapo ataweza kupata mkopo wa boda na kuondokana na adha ya kuajiriwa kwa kumiliki boda yake mwenyewe au kufungua biashara nyingine nje ya bodaboda na hivyo kujiongezea kipato.

Kuhusu fao la matibabu alisema bado wapo katika majadiliano na vyama vya boda ambapo alidai kwamba kutokana na usafiri huo kuwa mojawapo ya usafiri unaoongoza kwa matukio ya ajali kwa sasa itawasaidia kupata huduma za matibabu kwa uhakika pale inapotokea.

Awali akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, alisema mpango wa GEPF kulifikia kundi hilo unapaswa kuigwa kwa kuwa ni moja ya kazi ambazo serikali imeamua kuihalalisha.

Lyaviva alisema ni wakati wa Bodaboda kuchangamkia fursa hiyo ya kujiwekea akiba kwa kuwa ukweli ni kwamba hakuna anayejua kesho yake atakuwa katika hali gani ya kukosa uwezo wa kufanya kazi.

Kuhusu mafunzo alisema angependa kuona kuwa hakuna boda anayeruhusiwa kuingia barabarani bila cheti cha mafunzo ya usalama barabarani wala leseni.

Naye Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani, Mohammed Mpinga,, alisema katika mafunzo hayo, madereva wemeweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo usalama wa kujihami, namna ya kuikarabati pikipiki, muenekano wa dereva na somo la ujasirimali ambapo alidai wameshaanza kuona mabadiliko chanya kwa wahitimu hao.

Katibu wa waendesha boda, Daudi Laurian, alisema watahakikisha kampeni inayoanza Januari ya kutoruhusiwa boda wasio na mafunzo wala leseni, wanalisimamia wenyewe kwa kuwa limekuwa likiwaathiri hata ambao wanafuata taratibu.

Laurian alisema wanataka kuona wanauruka mwaka 2007 salama bila ya boda kuhusishwa na vitendo vya ujambazi wala ajali na kuongeza ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha hayo yanatimia jambo litakalosaidiwa pia na kufuata sheria.
Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva akizungumza na wamiliki na madereva pikipiki 500 juu ya kutojiingiza katika vitendo vya uhalifu ikiwemo kuwapora pochi abiria wao pamoja na kuwapakia majambazi kwa ajili ya kuenda kufanya uhalifu.leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza na wamiliki na madereva pikipiki 500 juu ya madereva wote wanatakiwa kutii sheria bila shuruti kwa wakati wote wanapokua barabarani ikiwa ni pamoja na kuvaa helment,kutokupakia mishikaki pamoja na kuendesha chombo wakiwa hawajalewa ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Maſao ya Kustaafu-GEPF Jacob Ondara akizungumza na wamiliki na madereva pikipiki 500 juu umuhimu wa kujiungaa na Mfuko wa huo ilikuweza kupata bima ya Afya kwaajili ya kupata matibababu kwa haraka, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Darasa la Kibaha,Akas Kiruwa katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Madara ya Mbalilmbli wa madereva wa pikipiki wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.
Madereva wa pikipiki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.

No comments: