Thursday, November 10, 2016

waomba kuundwa kwa sheria ndogo ndogo kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji mkoani Kigoma

Uharibu wa vyanzo vya maji.
 
Na Rhoda Ezekiel  Globu ya Jamii-Kigoma,

MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Elisha Bagwenya amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe kushirikiana na watendaji wake kuunda sheria ndogo ndogo zitakazo toa adhabu kwa baadhi ya wananchi wanao haribu vyanzo vya Maji kwa kufanya shughuli za kibinadam katika vyanzo hivyo hali inayo pelekea Halmashauri kukosa maji.

Rai hiyo aliitoa Jana katika kikao cha Baraza La madiwani wa Halmashauri hiyo Bagwenya alisema kumekuwa na Uhalibifu mkubwa katika vyanzo vya Maji unao sababishwa na wananchi wanaofanya shughuli zao katika vyanzo hivyo na kusababisha uchafuzi wa Maji na kupelekea wananchi kupata magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na kipindu pindu.

Alisema Mkurugenzi kwa kushirikiana na wataaramu kuunda sheria ndogo ndogo za uhifadhi wa misitu na mazingira ziletwe kwenye kikao zijadiliwe na  zipitidhwe na Halmashauri ilizianze kutumika na kusaidia vyanzo vya Maji kutunzwa na kuisaidia wananchi kupata Maji safi na Salama.

Hata hivyo Bagwenya alimuomba Muhandisi wa Maji Wilaya kuhakikisha wananweka dawa katika vyanzo vya Maji ilikuhakikisha wananchi na ambapo ya Maji yaliyo safi na Salama na kuweza kuepuka Magonjwa ya mlipuko yaliyo kuwa yakijitokeza kwa kipindi cha nyuma.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marko Gaguti alisema Serikali ya wilaya imeandaa Mpango wa kupitankatika kila kijiji kutoa maelekezo kuw Wananchi wote kufanya shughuli zao nje ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji ilkuweza kulinda vyanzo hivyo na wananchi waweze kupata Maji ya kutosha.

Gaguti alisema anaunga mkono wazomlq Halmashauri LA kuunda sheria ndogo ndogo za kutunza vyanzo vya Maji ilikulinda vyanzo vya Maji,alise mpaka sasa kijiji kinamiundombinu chini ya 68% ambapo Wananchi wengi wana kosa Maji upayikanaji wa Maji ni mdogo.

"Vyanzo vya Maji vinatakiwa kuachwa wananchi hawarusiwi kulima,kupanda miti au kufanya shughuli zozote katika mita sitini kuanzia kwenye vyanzo, Mkurugenzi anatakiwa kuwapa taarifa viongozi wa vijiji kulinda vyanzo hivyo na kuwachukulia hatua wrote watakao Keuka kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo", alisema Gaguti.

Sambqmba na hayo Gaguti alisema Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa hutuma za Afya Wilaya ni humo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Hospital ya wilaya ya Buhigwe , Halmashauri imeamua kuanza ujenzi wa Hospital I ya wilaya kwa kuchukua lamani ya Hospital ya Monduli na kupitia mapato ya ndani na michango kutoka kwa wadau watajenga hospital I hiyo iliwananchi waweze kupata Huduma Katibu.

Nae Kaimu muhandisi wa Maji Wilaya ya Buhigwe Muhanfisi Mwafrika Charse alisema Sheria namba 11 ya mwaka 2009 inasema watu hawa ruhusiwi kufanya shughuli zozote za kijamii mita60 kuanzia kwenye chanzo cha Maji ilikuhakikisha vyanzo vinalinda.

Alisema mikakati iliyopo ni idara ya Maji wilaya humo kuzungukia vijiji vyote vyenye vyanzo,  kutoka Elimu kwa Wananchi iliwaweze kupata Elimu ya kutunza vyanzo hivyo na kupata Maji ya kutosha na safi kwa kuepuka uhalibifu wa vyanzo hivyo.

No comments: