Taasisi
ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imezindua MPANGO Mkakati wa
miaka mitano 2016 – 2020 ambao umeainisha vipaumbele saba kwa kufanyia
Utafiti katika masuala mbalimbali ya Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Bi. Amina Shabani kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo
Doto M James.
Mpango
Mkakati huo 2016 – 2020 ambao ni wa sita tangu kuanzishwa kwa Taasisi
hiyo,umeainisha maeneo makuu saba ambayo ndani ya maeneo hayo kuna
maeneo mengine madogo madogo ishirini na sita ambayo kwa pamoja
yatatiliwa mkazo katika kipindi hicho cha miaka mitano.
Maeneo
hayo makuu ni; Kukuza Uchumi, Ajira na Viwanda; Utawala na Uwajibikaji;
Utandawazi na Ushirikiano wa kikanda; Utoaji wa huduma na ulinzi wa
kijamii; Mali asili na Usimamizi wa Mazingira; Usimamizi wa Maarifa na
Ubunifu pamoja na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi
Kida (wa pili kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za ESRF kwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban
(kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF kuzindua Mpango mkakati wa sita
wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020. Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF,
Charles Singili (kushoto) pamoja na Mshehereshaji wa uzinduzi wa mpango
mkakati huo, Prof. Samuel Wangwe (wa pili kushoto).(Picha na Zainul
Mzige wa Modewjiblog)
Bi.
Amina alisema kwamba serikali imefurahishwa sana na juhudi kubwa
zinazofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
kusaidia
serikali kusukuma mbele huduma zake kwa jamii na kupanua uwezo wa
kutengeneza Taifa linalotekeleza sera za ukuaji wa uchumi.
Aliwapongeza
waandaaji wa Mpango Mkakati huo na kusema Wizara yaFedha na Mipango
inafurahishwa sana na namna Taasisi hiyo kama chombo cha Utafiti
kinavyosaidia kuonyesha njia na kutoa mwelekeo kwa masuala mbalimbali ya
kisera na utekelezaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi
Kida (kulia) akiongozana na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano
katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na Mpango Mkakati huo, serikali
imefurahishwa kuona kuwa taasisi hiyo pia imejikita katika kusaidia
kuona serikali inafanikisha utekelezaji wa maendeleo endelevu nchini.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akizungumza kabla ya
kumkarisbisha mgeni rasmi Bi. Amina kuzindua Mpango Mkakati huo pamoja
na mambo mengine alisema kwamba Taasisi yake imejikita katika kufanya
tafiti maeneo saba ambayo yamo katika mpango wa pili wa maendeleo.
Wadau
katika kujadili Mkakati huo wameiomba Serikali kufanikisha Tafiti zote
zilizokusudiwa kufanywa zinatekelezwa kwa kuisaidia Taasisi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi
Kida akizungumza machache na kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na
wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa
miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ESRF.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akizungumza
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James kwenye uzinduzi wa
Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika hafla ya
uzinduzi huo.
Mtafiti
Mshiriki Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii
(ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Oswald
Mashindano akielezea wadau mbalimbali mambo muhimu yaliyomo katika
mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban
akikata utepe kuzindua rasmi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa
ESRF 2016-2020 huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya
wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban
(katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini
ESRF, Charles Singili (kulia) kwa pamoja wakiwa wameshika mpango mkakati
wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 mara baada ya kuuzindua rasmi
katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Pichani
juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi mpango
mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 wakipitia mpango
mkakati huo uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
mikutano wa ESRF.
Sehemu ya wadau, wageni waalikwa na wafanyakazi wa ESRF katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Pichani
juu na chini ni wageni waalikwa walioshiriki kwenye uzinduzi huo
wakitoa maoni juu ya mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF
2016-2020 mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili akitoa neno la shukrani kwa
mgeni rasmi na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango
mkatiti huo.
MC
ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya ufundi inayotoa ushauri kwa
menejimenti ESRF, Prof. Samuel Wangwe akizungumza jambo katika hafla ya
uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020
iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF, jijini Dar es Salaam.Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban
akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa
mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban
katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi
wa mpango mkatiti huo.
No comments:
Post a Comment