Na Dotto Mwaibale
UJUMBE
wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili
nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa
na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Akizungumza
na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara
ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa
chama hicho, Jia Bo.
Madabida
alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina
ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa
Taifa hilo Hayati Mao Tse-Tung.
Alisema
ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili
nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini
China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda
kujua kama wameyafanyia kazi.
Mratibu
wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka
China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.
"
Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu
na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba, Ulaya hasa
katika siasa za kijamaa" alisema Chana.
Alisema
wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika
maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza
mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi
waliyonayo.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida
(kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015, Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na
Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo,
Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita
kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
Mratibu
wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto), akizungumza na wajumbe hao.
Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.
No comments:
Post a Comment