Vyombo vya baadhi ya wakazi
wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtoni Kijichi jijini
Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia
nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na
Francis Dande).
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi ya kuwaondoa
wadaiwa sugu ambao wlinunua nyumba na
kushindwa kulipa deni lililobaki kwa muda uliopangwa.
Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu
Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo
ni za Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam ambapo alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa
wadaiwa saba.
“Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na
kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.
Aidha alisema kwamba wadaiwa hao
waliondolewa katika nyumba hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo
nyumba hizo zitauzwa kwa watu wengine.
Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu
kwa wale watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.
Shirika la NSSF limewataka walionunua ama
kupanga nyumba kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa
vyombo vyao nje na kupata hasara.
No comments:
Post a Comment