Tuesday, November 15, 2016

SENSEI KALONGA: SANAA YA KUJILINDA KWA MIKONO MITUPU (KARATE) NI TAALUMA

Na Woinde Shizza, Kilimanjaro 
Tamasha la kutunukiwa vyeti kwa wachezaji waliofuzu madaraja ya mikanda tofautitofauti limefanyika hivi karibuni katika manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Tamasha hilo limeandaliwa na chama cha karate mkoa wa Kilimanjaro huku ambapo zaidi ya vijana 54 wa kike 5 na wakiume 49 walishiriki katika mchezo huo,ambapo umeshirikisha vilabu viwili tofauti  ambavyo ni Mo town club na Suparampe zote zinatoka manispaa ya Moshi mjini.

Raisi wa Shirikisho la karate nchini Tanzania na mwenyekiti wa chama cha karate mkoani Kilimanjaro Sensei Kalonga amesema kuwa vijana hao wamepata mafunzo kwa  mwaka mmoja na ni utaratibu wa chama cha karate.
Kalonga amesema kuwa wameandika historia mpya kwa kuupigania mchezo wa karate mkoa wa kilimanjaro na Tanzania nzima, pia  umuhimu wa maendeleo ya vijana kupitia mchezo wa Karate,amesema mchezo huo ni taaluma ndiyo maana wamekaa darasani na kufuzu.
"Tumieni mafunzo mliyoyapata vizuri mahali popote mtakapokuwepo zingatieni nidhamu ,upendo pamoja na maadili yote mliyofundishwa huku mkiwa mfano bora wa kuigwa katika jamii, nyie ndio mkataokuwa barua ya kusomeka kwa jamii kuwa karate siyo mchezo wa kihuni
Makamu mwenyekiti wa cha Karate mkoani Kilimanjaro Sensei Hamza Mzonge amesema kuwa karate siyo mchezo wa kihuni kama baadhi ya watu wadhaniavyo,bali msingi mkuu wa Karate ni Nidhamu, moyo safi, na kuiheshimu jamii  pamoja na familia kwa ujumla.

Sensei Hamza amesema kuwa karate inatengeneza afya, kudumisha nidhamu,karate haitumiki kuvunja nidhamu ,bali ni mchezo kama michezo mingine na unakanuni zake ,ni tofauti na vile ambavyo watu wandhania lazima uheshimiwe na kila mwanakarate.
"Tunaposema karate haina kufuzu ni kweli ,maana mie mwenyewen ni mkufunzi lakini hadi leo bado naendelea kujifunza siku zote,tudumishe nidhamu,mtu yeyote yule anayevunja nidhamu katika karate siyo katateka alisisitiuza sensei Hamza.
Kwa upande wake sensei Ibrahim Mganga amewataka wahitimu hao kuwa mfano bora haswa katika kuwa na moyo safi huku alisisiktiza kuwa karate ni nidhamu na moyo safi ndiyo sababu huwa wanavaa mavazi meupe kama ishara ya usafi.
"tunavaa mavazi meupe hili vazi linaonyesha usafi na mara zote ukivaa nguo nyeupe utajilinda ili usilitie doa maana litaonekana na kuweka dosari,hivyo basi karate ni zaidi ya vazi jeupe msitumie karate vibaya ikaja ikaonekana ni ya ovyo ndiyo sababu karate siku zote msingi wake ni NIDHAMU"alisisitiza sensei Ibrahim.

Rais wa Shirikisho la Karate nchini Tanzania ambaye pia ni mwenyekitti wa chama cha Karate mkoani Kilimanjaro Sensei Geofrey Kalonga


 Hamza Mzonge ambaye ni kaimu mwenyekiti wa chama cha karate mkoa wa Kilimanjaro
 Sensei Hamis Wembo Katibu mkuu mtendaji wa chama cha karate mkoa wa Kilimanjaro pia ni mkufunzi wa jeshi la polisi mkoani hapo.
Sensei Ibrahim Mganga ambayaye ni mkufunzi wa chuo cha polisi Moshi  


Aliyepo katikati ni rais waShirikisho la Karate nchini Tanzania ambaye pia ni mkufunzi wa Goju Ryu Karate Mkoa wa Kilimanjaro Sensei Geofrey Kalonga, wa kwanza kulia ni Sensei Hamis Wembo ambaye ni mkufunzi wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Katibu mkuu wa Chama cha Karate mkoa wa Kilimanjaro,aliyepo kulia kwake ni Mkufunzi wa chuo cha polisi Moshi( CCP)Sensei Ibrahim Mganga , wakiwa katika tamasha la kuwatunuku vyeti wanafunzi wa katare waliofuzu mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi Mjini.Picha na Vero Ignatus Blog.
Sensei Hamza Mzonge ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama cha Karate mkoa wa Kilimanjaro akitoa maelekeza kwa wahitimu mafunzo ya mchezo  wa Karate Mkoa wa kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus blog.
Club mbili za Karate wakiwa katika maonyesho ya pamoja katika tamasha lilifanyika katika shule ya msingi mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi mjini,ambazo ni Mo town Club na Suparampe club zote za Moshi  mjini.Picha na Vero Ignatus Blog.

Wahitimu wa mafuzo ya karate wakionyesha yale waliyojifinza kabla ya kukabiddiwa vyeti vyao hapo pia wakina dada wamo ndani wakionyesha kata mbalimbali.Picha na Vero Ignatus Blog.


Mwanadada Matilda Mallya akifanya yake katika karate kwenye tamasha hilo la kukabidhiwa vyeti kwa wahitimu lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi mjini ambapo yeye alipewa cheti kwa kufuzu mafunzo ya mkanda wa brown. Picha na Vero Ignatus Blog.



Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Karate akipokea cheti chake katika tamasha lililofanyika katika shulke ya msingi Mwenge iliyopo manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro .

No comments: