Na
Ally Daud-MAELEZO
Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia
Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla ameongoza kikosi kazi katika msako wa
Viwanda vinavyotengeneza pombe Kali feki ikiwemo viroba na zinginezo na
kufanikiwa kukamata kiwanda feki kilichopo maeneo ya sinza jijini Dar es salaam.
Akiingoza msako huo Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.
Hamis Kigwangalla amesema kuwa msako huo
unaofanywa na Wizara hiyo inashirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA umefanikiwa kukamata kiwanda feki
kinachotengeneza pombe aina ya viroba, konyagi, Smirnoff na zedi kilichopo
sinza jijini Dar es salaam.
"Tunafanya msako huu kwa kushirikiana na
kikosi kazi cha Serikali ili kuondoa
pombe haramu zinazotengenezwa kiholela
na kwa kutozingatia viwango vya
ubora kwa maendeleo na Afya ya
watanzania" alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha Dkt. Kigwangalla ameongeza kuwa katika msako
huo wamefanikiwa kukamata kiwanda hicho kikiwa na nyenzo za kutengenezea pombe
haramu kama vile chupa za konyagi,
vifuniko, lebo, vifuko na nyenzo zingine za kutengenezea pombe hiyo haramu.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa msako huo umebaini
kwamba watengenezaji hao wanatumia gongo na spiriti kutengeneza pombe kali kitu
ambacho ni hatari kwa afya ya watanzania hususani vijana hivyo kufanya nguvu ya
taifa kupotea.
Katika msako huo pia ulifanikiwa kukamata maduka yanayouza pombe hizo maeneo ya Mwenge
na Manzese jijini Dar es salaam ikiwa chini ya msambazaji Bw. Yusuf Yusuf Abdul
Kalambo mkazi wa Kimara ambaye anatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya
upelelezi zaidi.
Aidha Dkt. Kigwangalla ameamuru wauzaji wa maduka
hayo wafunge maduka yao mara moja na kushikiriwa na Polisi mpaka pale upelelezi
utakapokamilika ili sheria stahiki ifuate mkondo wake aidha kulipa faini au
kufutiwa leseni za biashara.
Zoezi hilo la kusaka Viwanda feki vinavyotengeneza
pombe kali linafanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TFDA pamoja na
jeshi la polisi ni endelevu mpaka bidhaa feki zitapotoweka nchini.
Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akikagua baadhi ya pombe kali katika moja ya duka alilolikamata lililopo mwenge Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla katikati akimuhoji muuza duka la pombe kali ambazo ni feki lilopo Manzese Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla wa kwanza kulia akiwa ameshika beseni lililojaa vizibo vya konyagi katika kiwanda feki kilichokamatwa maeneo ya sinza Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini kushoto ni Afisa kutoka TFDA.
Baadhi ya nyenzo za kutengenezea pombe kali ambazo ni feki aina ya konyagi katika kiwanda feki kilichokamatwa maeneo ya sinza jijini Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
Baadhi ya pombe kali aina ya konyagi na amarula ambazo ni feki zilizokamatwa katika duka la kuuza pombe kali lililopo manzese jijini Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
No comments:
Post a Comment