Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MASHINDANO ya kuchezea mpira (Football Freestyle) yaliyoandaliwa na chama cha mchezo huo Freestyle Football Tanzania (FFT) yanatarajiwa kuanza Novemba 19 kwa Wilaya tatu za Jiji la Dar es Salaam Temeke, Ilala na Kinondoni na uzinduzi wa shindano hilo unatarajiwa kuanzia kwenye viwanja vya Mwembe Yanga.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo unayodhaminiwa na kinywaji cha Red bull ikishirikiana na Clouds TV kupitia kipindi cha Sports Bar anatarajiwa kuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.
Akizungumza na Mratibu wa shindano hilo Jacob Mbuya amesema kuwa washiriki wa shindano hilo watajiandikisha bure na washiriki wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 15 na kuendelea huku fomu za ushiriki zinapatikana Clouds TV na Ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni pamoja na mitandao ya kijamii kupitia kurasa zao.
Mashindano yanatarajiwa kuanzia Wilaya ya Temeke Novemba 19 na kutapatikana washiriki watano na baadae kuhamia kwenue wilaya ya Ilala ambayo pia itatoa washiriki watano huku Kinondoni ikitoa sita ambao wataingia Fainali itakayochezwa Coco Beach, Disemba 11 na kwa upande wa Wilaya ya Ilala shindano hilo litafanuyika kwenye viwanja vya Boma, Novemba 26 kabla ya kuelekea Kinondoni kwenye uwanja wa Tp Sweet Corner, Disemba 3. Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Pascal Chang'a amesema kuwa wameamua kuanza kufanya mashindano haya na kupata vipaji ambao watawapa fursa ya kwenda kimataifa zaidi kwani huwezi kwenda kushiriki kama hujafanya nchi kwako na alitaja baadhi ya sheria za mchezo huo kuwa ni kila mshiriki atapewa sekunde 30 za kuchezea mpira, mchezaji atakuwa peke yake jukwaani na pia akidondosha mpira atakuwa amepoteza pointi.
Naye Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy amesema kwua wameamua kushirikiana na FFT ili kuweza kuibua vipaji vya vijana katika mchezo huu na pia wao wamedhamini kwa kila kitakachokuwa kinahitajika.
Katibu
wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey akizungumza na
waandishi wa habari wakati kuhusiana na mashndano ya kuchezea mpira
yanayotarajiwa kuanza Novemba 19, kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans
Oysterbay Drinks, Hanson Heddy na kulia ni Mratibu wa Shindano hilo Jacob
Mbuya.
Mratibu wa
Shindano la kuchezea mpira Freestyle Football Jacob Mbuya akizungumza na
waandishi wa habari na kutoa utaratibu wa ushiriki kwa vijana kuanzia miaka 15
na kuendelea kulia ni
Katibu wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey
kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy na
mwisho ni Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Pascal Chang'a. Picha
na Zainab Nyamka.
No comments:
Post a Comment