Monday, October 31, 2016

WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WILAYA YA ILALA WAPEWA SEMINA ELEKEZI

WENYEVITI wa Halmashauri ya wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam wamekutana Wilayani Bagamoyo katika Semina maalum ya kujengeana uwezo na uwelewa ikiwamo kutambua majukumu yao kwa lengo la kuepusha migongano kati ya Wenyeviti,Watedaji pamoja na Madiwani.

Akizungumza wilayani humo mara baada ya kufungua semina hiyo Mwenyekiti wa Wenyeviti mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti Wilaya ya Kinondoni Juma Zubery amepongeza hatua ya wenyeviti wa wilaya ya Ilala kuona kuna umuhimu wa kufanya semina ya kukumbusha na kuelekezana majukumu ya wenyeviti katika mitaa mbalimbali ili kuepusha migongano kati yao na watendaji wengine wa Serikali.

Zubery amesema uendeshaji wa Serikali za mitaa una changamoto kubwa ikiwamo viongozi wengi kushindwa kujua mjukumu yao hali inayosababisha kutofautiana mara kwa mara miongoni mwao na kufikia hatua ya mtendaji wa mtaa na mwenyekiti  kugombea hata mihuri jambo ambalo kimsingi linatokana na uelewa mdogo wa kutojuwa mipaka ya kazi zao.

Kwaupande wake Menyekiti wa Wenyeviti katika Manispaa ya Ilala Ubaya Chuma amewataka wenyeviti hao kuogopa kutumia mihuri ya watendaji wa mtaa huku akidai kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria na  hivyo kukaribisha migongano miongoni mwao. 

Katika Semina hiyo wenyeviti zaidi ya 44 kutoka Halmashuri hiyo wamekutana huku wakimomba Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo kama hayo kwa wenyeviti wote wa Serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam Juma Zubery Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Semina elekezi kwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa wilaya ya Ilala ambapo lengo la semina hiyo ilikuwa ni kuwajengea uwezo na uwelewa juu ya majukumu yao.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mogo, Geoge Mtambalike akitoa mada ya ulinzi na usalama katika semina hiyo ya wenyeviti wa serikali ili kujuwa namna ya kuweza kukabiliana na vitendo vya kiarifu katika mitaa yao.

Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma akiwasilisha mada mbele ya wajumbe ambao ni wenyeviti wa Serikali za mitaa mbalimbali wilayani humo ambapo alijikita katika kutoa elimu ya kutambua majukumu yao nakuacha kumbea mihuri huku akidai ni makossa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kuchukua mhuhuri wa mtendaji wa mtaa au kata.

Wenyeviti wa Serikali za mitaa mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya ilala wakisikiliza kwa makini mada ambayo ilikuwa ina tolewa na mtoa mada,Ubaya Chuma kuhusu wenyeviti hao kuona kwamba wanajukumu kubwa la kulinda usalama wa maeneo yao ikiwa pamoja na kuimarisha vikundi vya ulinzi na usalama.
Katibu Tawala wilaya Bagamoyo Mjini Doris Mwakitobe akizungumza jambo wakati wakufunga semina ya wenyeviti wa serikali za mitaa mbalimbali wilaya ya Ilala,ambapo katika kufunga semina hiyo aliwataka kwenda kutumia mafunzo hayo kufanya kazi kwa bidi na kwa kuzingatia kauli mbiuya rais ya Hapa kazi tu kulia ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mogo Geoge mtambalike.
Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

No comments: