Kabla ya mpambano Abubakari Soud ‘Amigo’ wa Jahazi alipanda jukwaani kuwanogesha mashabiki.
Mtangazaji
wa Redio Times FM, Aisha Mbegu (kulia) akirusha sarafu ili kumpata
mwanamuziki wa kuanza kukamua kati ya Leyla na Isha. Kushoto ni
mshereheshaji MC wa Jahazi, Mwasity Robert, na katikati ni mwakilishi wa
Isha na Leyla.
Baada ya Isha kuanza kukamua shabiki huyu alikunwa na hivyo kuvamia jukwaa kwenda kumtunza.
Sehemu ya umati uliofurika ukumbini hapo kufuatilia mpambano huo.
Leyla akifanya yake baada kupanda jukwaani.
Mtangazaji na MC wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu wa Redio Times FM, uzalendo ulimshinda na kuanza kubanjuka.
Wanenguaji wa Jahazi wakimsindikiza Leyla.
Leyla akiwanogesha mashabiki.
Isha Mashauzi aliyevamia tena jukwaa akiwa katika na vazi jingine.
Isha na kundi lake wakishambulia jukwaa.
Wakati
Isha akipagawisha mashabiki, Leyla alikunwa na kumvamia Isha jukwaani
na kumtunza hali iliyosababisha mayowe ya kushangilia.
Uhasama wao ulikuwa ni jukwaani tu, kwani baada ya kushuka jukwaani wote walikuwa kitu kimoja.
MASHABIKI
wa burudani, hususan muziki wa taarab, usiku wa kuamkia jana walipata
burudani ya aina yake wakati wakali wa muziki huo, Isha Mashauzi na
kundi lake la Mashauzi Classic kwa upande mmoja na Leyla Rashid kwa
upande mwingine akiwa na kundi lake la Jahazi Modern Taarab,
walipotoana kijasho kwenye onesho maalum la kutaka kujua nani mkali
kati yao.
Kabla
ya mpambano huo kulikuwa na ubishani mkali kwa mashabiki ambapo upande
fulani ulisema Isha ndiye mkali kuliko Leyla huku wengine wakisema
“aaah, wapi bwana Leyla ndiyo mkali zaidi; pale Isha haingii hata kwa
nini”!
Hatma
ya ubishi huo ni mpambano uliowakutanisha wawili hao na kuwaacha
mashabiki wakijionea na kuamua wenyewe. Kabla ya wakali hao kupanda
jukwaani mshereheshaji wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu, wa Redio Times
ilibidi arushe sarafu hewani ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kulivamia
jukwaa maana walianza kutegeana. Baada ya sarafu kurushwa Isha ndiye
aliyeangukiwa na zali la kuanza kuonesha mavitu vyake jukwaani.
(PICHA/HABARI: RICHARD BUKOS /GPL)
No comments:
Post a Comment