Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba, Sultan
Pwaga ( wa pili kutoka kulia mbele) akimwongoza Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ( wa tatu kutoka
kulia mbele) kwenye ziara ya kukagua kituo hicho ili kujionea shughuli
zake.
Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba, Sultan
Pwaga akielezea shughuli za kiwanda hicho mbele ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani).
Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba, Sultan
Pwaga (kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) katika ziara hiyo.
Eneo la mwanzo la bomba la kusafirisha gesi kuelekea Dar es Salaam
kupitia Mtwara, Lindi na Pwani kama linavyoonekana pichani.
Sehemu ya kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba kama
inayoonekana pichani.
Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba, Sultan
Pwaga (kushoto) akitoa maelezo hukusu mikakati inayofanywa na
kiwanda hicho katika kuhakikisha kuwa gesi ya uhakika inapatikana kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa
(kulia).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika chumba cha
kuongozea mitambo (control room) katika kiwanda cha kuchakata gesi
cha Madimba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa
(kushoto) akifuatilia maelezo ya namna ya uendeshaji wa mitambo ya
kuchakata gesi ya Madimba yaliyokuwa yanatolewa na Stanslaus
Malya (hayupo pichani).
Mtaalam kutoka kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba, Stanslaus
Malya akionyesha uongozwaji wa mitambo unavyofanywa katika
kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa
(waliokaa mbele katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo
ya Petroli Nchini (TPDC) Kapuulya Msomba ( kushoto waliokaa mbele)
wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa kiwanda cha kuchakata
gesi cha Madimba na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na TPDC.
No comments:
Post a Comment