Mshambuliaji Themi
Felix, alianza kuishtukiza Azam FC kwa kuifungia bao la uongozi Kagera
Sugar dakika ya 32 kabla ya Mudathir Yahya kusawazisha kwa bao zuri la
shuti akimalizia pasi ya kichwa aliyodondoshewa na Bocco kufuatia faulo
iliyochongwa na Erasto Nyoni.
Hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha
pili Azam FC ilikianza kwa kasi kubwa ikitaka kupata bao la uongozi
lakini mabeki wa Kagera Sugar walikuwa kizuizi kikubwa kwa washambuliaji
wa mabingwa hao wakiokoa hatari zote.
Mwamuzi wa mchezo wa leo,
Mathew Akrama kutoka Mwanza, aliamuru penalti ipigwe langoni mwa Azam
FC baada ya beki Aggrey Morris kumfanyia madhambi Ally Nasoro ndani ya
eneo la hatari, na penalti hiyo ilifungwa na Felix.
Baada ya bao
hilo, mabadiliko ya wachezaji watatu yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Azam
FC kwa nyakati tofauti ya kuwatoa Gonazo Ya Thomas, Gadiel Michael na
Jean Mugiraneza na kuingia Shaaban Idd, Frank Domayo na Khamis Mcha,
yaliongeza uhai kwa timu hiyo na kupelekea kufunga mabao mawili
yaliyoipa ushindi huo.
Alianza Domayo dakika ya 80 aliyefunga
bao zuri kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la 18 akimalizia mpira
uliotemwa vibaya na mabeki wa Kagera Sugar kabla ya Bocco kufunga la
ushindi dakika sita baadaye akifunga kwa kichwa safi kufuatia krosi
iliyochongwa na Shaaban Idd.
Bao hilo linamfanya Bocco kufikisha
mabao matano kwenye msimu huu wa ligi akizidiwa mabao mawili na Shiza
Kichuya wa Simba, anayeongoza kileleni kwa mabao saba.
Timu zilivyokuwa zinaingia Uwanjani
Kikosi cha Azam Fc
Kikosi cha Azam Fc leo kilikuwa:
Aishi
Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/Khamis Mcha dk 79, Aggrey Morris,
Daniel Amoah, Jean Mugiraneza/Frank Domayo dk 70, Ramadhan Singano,
Salum Abubakar, John Bocco (C), Mudathir Yahya, Gonazo Ya Thomas/ Shaaban
Idd dk 62
Mashabiki wakiwa na Jazba kubwa Uwanjani Kaitaba
Mashabiki wa Kagera Sugar wakiwa na Mabango wakionesha ujumbe wao kwa Timu yao inayoongozwa na Maxime.
Wakidai kuwa ana Tabia ya kuuza Mechi.
Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakijiuliza
Kichapo cha pili mfululizo
Waamuzi wa Mtanange huo
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa na Ujumbe wao
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar
Juu kwa juu Wanahabri wa Azam Fc wakichukua Picha
Bocco tena
Penati.... mpira ukipangwa
No comments:
Post a Comment