Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TIB Corporate Bank , Bw Frank Nyabundege (Kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa
Bohari Kuu ya Dawa nchini, Bw Laurean Bwanakunu ambae taasisi yake ni mteja wa
benki hiyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani
iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dae es Salaam jana ili kutoa fursa
kwa wateja wake kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Wafanyakazi
wa TIB Corporate Bank , wakimpokea mmoja wa wateja wakubwa wa benki
hiyo,Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya PMM Estate (2001), Dr Judith
Mhina (kulia) alipohuduhuria hafla fupi ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ili kutoa fursa kwa wateja wake kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Meneja Uhusiano wa Benki ya TIB Corporate, Margareth
Mulenga (kushoto) na Ofisa wa benki hiyo Jane Magingi (katikati) wakisalimiana
na mmoja wa wateja wakubwa wa benki hiyo,Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni
ya PMM Estate (2001), Dr Judith Mhina (kulia) alipohuduhuria hafla fupi ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ili kutoa fursa kwa wateja wake kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo
Katika
kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani,TIB Corporate Bank
imekutana na wateja wake ili kujadili nafasi na mchango wa benki hiyo
katika biashara huku ikitoa nafasi kwa wateja na wadau wa benki hiyo
kutoa ushauri kuhusiana na huduma zake.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana wakati hafla fupi iliyoambatana na mazungumzo
hayo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw Frank Nyabundege
alisema maadhimisho hayo ambayo ni ya kwanza kufanywa na benki hiyo
tangu ianzishwe mwaka 2015 yametoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kutoa
mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
“Maadhimisho
haya ya wiki moja yalianza Octoba 3 mwaka huu na tunatarajia
kuhitimisha Oktoba 7, kweli yamekuwa na manufaa makubwa sana kwetu kwa
kuwa tumeweza kukutana na wateja pamoja na wadau wetu mbalimbali ambao
wametumia fursa hii kutupatia mrejesho kuhusiana na huduma tunazotoa,’’
alibainisha.
Bw
Nyabundege aliongeza kwamba kwasasa benki hiyo imeboresha zaidi huduma
zake ikiwemo suala la mikopo mikubwa na midogo huku akitoa wito kwa
mashirika ya umma, watu binafsi na taasisi mbalimbali kujiunga na benki
hiyo.
“Kasi
yetu inachochewa zaidi na kauli mbiu ya Mh. Rais John Magufuli ya ‘hapa
kazi tu’ inayoenda sambamba na kuhimiza maendeleo ya viwanda na ndio
maana miongoni mwa mwa huduma tunazotoa ni pamoja na mikopo kwa ajili ya
viwanda,’’ alisema.
Kwa
mujibu wa Bw Nyabundege benki ya TIB Corporate kwa sasa ina wateja
takribani 12,000 huku ikitarajia kuvutia zaidi makampuni na taasisi
(corporate clients) kutumia benki hiyo, hatua aliyoitaja kuwa
itafanikiwa kupitia uwepo wa huduma bora katika benki hiyo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa nchini, Bw
Laurean Bwanakunu ambae taasisi yake ni mteja wa benki hiyo alisema
aliipongeza benki hiyo kwa kutoa huduma bora huku akiahidi kuwashawishi
mashirika mengine ya umma kujiunga na benki hiyo.
“Binafsi
nafarijika sana kuona kwamba taasisi yangu ambayo ni umma inafanya kazi
na taasisi ya fedha ya umma tena kwa ufanisi mkubwa ndio maana naahidi
kuwashawishi wenzangu ili waje kwa wingi kuunga mkono jitiahada za
serikali katika kuboresha taasisi zake za fedha,’’ alisema.
Ili
kuwaongezea wigo wa kibiashara wateja wake, benki hiyo hivi karibuni
iliingia mkataba wa ubia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) unaoiwezesha
benki hiyo kutoa huduma zake kupitia matawi makubwa 30 na madogo 30 ya
benki ya Posta yaliyopo kote nchini.
Hivi
karibuni pia benki hiyo ilifungua tawi lake kwenye ofisi za Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) ikilenga kusogeza huduma zake kwa ubora zaidi
katika bandari hiyo.
No comments:
Post a Comment