Friday, September 16, 2016

WATU TANO WANAODAIWA MAJAMBAZI WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi wa Habari juu opreresheni ambazo zimefanyika na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kamada wa Polisi wa Kanda Maalum, Kamishina Simon Sirro amesemaa askari Polisi wakiwa katika ufuatiliaji maeneo ya Goba Wilaya ya kipolisi Kawe Mkoa wa Kinondoni walimkamata mwanamke mmoja mkazi wa Goba, baada ya kupata taarifa kuwa anawafahamu majambazi wanaojihusisha na uvamizi kwenye maduka makubwa.
Amesema Katika na mwanamke huyo mahojiano aliwataja washirika wake watano  ambao walifuatiliwa na kukamatwa katika upekuzi walipatikana na silaha moja Bastola aina ya Browning TZCAR No.87881 ikiwa na risasi 17.
Sirro amesema katika mahojiano zaidi watu hao walikiri kufanya matukio ya ujambazi wa kutumia silaha jijin Dar es Salaam na mmoja wao alitaja silaha  nyingine amezifichwa kwenye majaruba ya Chumvi maeneo ya Ununio na kuwaongoza askari hadi kwenye eneo husika. walipofika maeneo hayo mtuhumiwa alianza kukimbia kuelekea kichakani ndipo Askari walirusha risasi iliyompata mguu wa kushoto  na kufanikiwa kumkamata.
Hata hivyo mtuhumiwa alifariki akiwa njiani kuelekea hosptalini kutokana na kuvuja damu nyingi kutokana na jeraha la risasi.
Aidha kati ya watuhumiwa wengine waliobaki mmoja aliwaongoza askari hadi eneo la gongolamboto anakoishi ambapo katika upekuzi
alipatikana silaha nyingine aina ya Shotgun Pump action ambayo imefutwa namba za usajili, msumeno mmoja na tupa moja  ya kunolea misumeno na visu.
Watuhumiwa wote wanne wanaendelea kuhojiwa mara ya upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Katika tukio lingine Polisi kanda Maalum Dar es salaam huko magomeni mtaa wa makumbusho  askari wakiwa doria  waliwatilia mashaka watu wawili wakiwa wamepakizana kwenye Pikipiki na begi dogo mgongoni ndipo askari waliwasimamisha hawakutii amri hiyo, Polisi walifuatilia ili kuwahoji  lakini watu hao baada ya kugundua kuwa Polisi wanawafuatilia walianza kukimbia kwa kasi mara wakatupa begi hilo, askari waliliokota baada ya  kulipekua begi hilo walikuta Bastola mbili aina ya Browning No, NE984517CAT5802  Ikiwa na risasi 11 na nyigine yenye No. CZ 2075 aina ya RAMI ikiwa na risasi 21 na magazine mbili iliyotengenezwa CZECH REPUBLIC jitihada ya kuwasaka watu hao zinaendelea.



Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam anatoa wito kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa kupitia kamati za ulinzi na usalama za mitaa kuimarisha ulinzi na usalama  katika maeneo yao na kutimiza wajibu wao, amewataka wamiliki wote wa nyumba jijini kuhakikisha kuwa wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu jijini.

Aidha amewataka kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na wao kuwa na picha za wapangaji wa nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuweza kuwabaini wahalifu mbalimbali katika maeneo yao, atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani.
  
Kikosi Maalum cha Kupambana na wezi wa magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam ililipokea taarifa toka kwa raia mwema kuwa kuna gari aina ya Toyota Carina T 289 DFL imeibiwa jijini DSM maeneo ya Kimara na kupelekwa mafichoni Mjini Mbeya. Baada ya taarifa hizo kupokelewa ndipo ufuatiliaji ulianza na  mtuhumiwa Mzawari Ahmad (29) mkazi wa mwananyamala alikamatwa jijini MBEYA akiwa na wenzake  wawili na alikiri kuhusika na tukio hilo.

Jeshi la polisi lilipata  taarifa toka kwa raia mwema kwamba huko Mkoa wa Kilimanjaro kuna gari nyingine aina ya Suzuki Carry T234 DAJ ambayo iliibwa maeneo ya Tandale jijini DSM mali ya NURDIN MPELEMBE. Askari walisafiri mkoa tajwa tarehe 05/09/2016 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Serafin Valerian(46), mfanyabiashara, mkazi wa Himo Kilimanjaro akiwa na magari  matatu ya wizi nyumbani kwake. Magari hayo ni:  SUZUKI CARRY T935 CPC rangi nyeupe namba zake halisi ni T139 DEK mmiliki ni BRAYAN LYIMO wa Ilala mtaa wa Arusha Dsm, gari nyingine ni TOYOTA RAV 4 rangi ya silver T732 CHP ambayo iliibwa kimara jijini Dsm tarehe 11/01/2016 nyumbani kwa CECULAR JAMES LAURICH namba halisi ni T440CAW.

 Mtuhumiwa  baada ya kupekuliwa alipatikana na hati mbalimbali za magari na pikipiki ambazo ni: kadi za bajaji, bima za magari mbalimbali yaliyopata ajali na kulipwa, plate namba za pikipiki, motorvehicle licence na TIN namba zenye majina mbalimbali.

watuhumiwa wote wakiwemo madalali wa magari haya ya wizi wanaendelea kutafutwa na mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano mara upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani.

polisi kanda maalum d’salaam yakusanya milioni tsh 882,570,000/= tozo za makosa ya usalama barabarani kuanzia Septemba 6 hadi septemba 16.

No comments: