Friday, September 16, 2016

SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA KOZI NA. 22 ZAFANA CHUO CHA MAGEREZA, TUKUYU MKOANI MBEYA

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(katikati) katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016(hawapo pichani) katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo leo Septemba 16, 2016 Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya.  Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Koplo wa Jeshi la Magereza Askari Mhitimu wa Mafunzo hayo kwa niaba ya wenzake.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) katika jukwaa kuu na Mgeni rasmi wakifuatilia maonesho mbalimbali ya kujihami askari kama wanavyoonekana katika picha.
 Gwaride la Wahitimu likipita mbele ya jukwaa kwa heshima


 Paparazi: Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakichukua matukio mbalimbali kutoka Uwanja wa gwaride kama wanavyoonekana.
 Onesho la kijasiri kama inavyoonekana katika picha ambapo mwendesha pikipiki ameweza kupita kwa juu usawa wa tumbo huku askari hao wakiwa wamejilaza chini bila uoga.
 Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016 wakishangilia kwa makofi mara baada ya kufungwa rasmi mafunzo hay oleo Septemba 16, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba yake ya kufunga rasmi kwa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya. Picha zote na Lucas Mboje wa Magereza.

No comments: