Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya
Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu akitoa maelekezo ya awali kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwalipa fidia wanufaika wote
Watendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya
Shanta Gold Mine Ltd wakifanya maandalizi ya malipo hayo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Baadhi ya wananchi wakisubiri maandalizi yakamilike ili wakabidhiwe mlungula wao
Dear Mama Exp ndio ndinga iliyotumika kuwafikisha wananchi hao eneo la tukio la kukabidhiwa cheki za malipo kwa wanufaika wote wa Mradi huo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu akizungumza na Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV Elisante Mkumbo kuhusu mchakato wa malipo utakavyo wanufaisha wananchi kupoitia mradi wa uchimbaji madini ya Dhahabu
Bi Juliana Kidamwe mkazi wa Kijiji cha Mlumbi akihakiki malipo yake kabla ya kukabidhiwa mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson
Kushoto ni mwasibu wa Shanta Gold Mining Ltd Caroline na Mwanasheria wa kampuni ya Shanta Gold Mining David Rwechungura wakikagua fomu zote za wanufaika kabla ya kuanza zoezi la kuwapatia cheki wanufaika wote wa Mradi huo
Meneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida
Philbert Rweyemamu akitoa maelekezo kwa wanufaika wote ya namna mchakato mzima utakavyokwenda
Kizito Ramadhani mkazi wa Kijiji cha Mlumbi akikagua fomu za malipo yake mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson kabla ya malipo
Kutoka kushoto ni Andrea Mtarim Mwenyekiti wa kijiji cha Kinyamberu, Ramadhani Mkuki Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlumbi, Selemani Hema Mtendaji wa Kijiji cha Mlumbi,na Jumanne Gwaye Mtendaji wa Kata ya Mang'onyi wakifatilia kwa makini zoezi la ulipaji fidia
Kushoto ni Meneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida
Philbert Rweyemam na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Male Samson wakisisitiza jambo wakati wakizungumza na wanufaika.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelezo ya malipo yao
Meneja wa
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida
Philbert Rweyemamua akikusanya vitambulisho kwa wananchi waliofika ili kurahisisha zoezi la malipo yao
Wanufaika wakipongezana mara baada ya kukamata cheki zao kwa ajili ya malipo ya fidia
Na Mathias Canal, Singida
Katika
miezi miwili ijayo kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold
Mining Limited) iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya
Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida huenda ikaanza uchimbaji wa
madini ya dhahabu baada ya kuanza kulipa fidia ya zaidi ya Milioni mia nane
(800,000,000) wanufaika awamu ya kwanza.
Malipo
hayo yamekabidhiwa kwa wahusika ikiwa ni siku tatu tu zimepita tangu Meneja wa Mradi
huo Philbert Rweyemamu alipotoa ahadi ya kuwalipa mwishoni mwa wiki hii
ili kupisha shughuli za uchimbaji kuanza.
Wanufaika
waliolipwa fedha hizo ni wale ambao wanatokanana na mazoezi mawili ya uthamini
yaliyofanywa kwenye eneo la mradi kwa ajili ya upanuzi wa kambi.
Hafla ya
malipo hayo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambapo wananchi 39 wamejipatia kitita
chao huku wengine wakishindwa kufika hivyo watakabidhiwa malipo yao wakati
watakapoyahitaji.
Malipo
hayo yanakamilisha umiliki wa maeneo hayo kwa Kampuni ya Shanta Gold mining kwa
ajili ya uchimbaji na kuwafanya wananchi hao kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu
pasina kinyongo chochote.
Akizungumzia
mchakato huo wa malipo hayo Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya
Shanta Gold Mine Ltd mkoani Singida Philbert Rweyemamu amesema kuwa umefika
wakati wa wananchi wa Wilaya ya Ikungi na taifa kwa ujumla kunufaika na mradi
huo utakaoongeza Wigo ya ajira na mzunguko mkubwa wa pesa utakaotokana na wingi
wa watu watakaodhuru Mkoani Singida kwa ajili ya shughuli za kazi.
Rweyemamu
alisema kuwa Mradi huo utakuwa na mahusiano chanya kwa wananchi kwani pamoja na
kuchelewa kuanza kwa uchimbaji lakini imeshiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Mang’onyi ulioanza mwezi May 2013
na kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2014 na hatimaye
kuzinduliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Parseko V. Kone.
Akielezea ujenzi
wa Kituo hicho Rweyemamu alisema kuwa Kituo hicho kimegharimu kiasi cha
shilingi milioni mia mbili ishirini na tisa, laki tisa sabini na sita elfu na
mia mbili thelathini (229,976,230) huku lengola ujenzi huo likiwa ni kwa ajili ya kusogeza
huduma ya usalama karibu na wananchi.
Naye Mwanasheria wa
Mradi huo wa uchimbaji Madini ya Dhahabu mkoani Singida David Rwechungura amesema
kuwa Hadi sasa Shanta imewekeza takribani dola za Marekani milioni ishirini na
tano hapa Singida yaani bilioni hamsini za fedha za Tanzania na bado gharama za
kujenga mgodi ambazo hazitapungua dola milioni mia moja.
Alisema Mgodi wa Shanta huko Chunya Mkoani Mbeya unazalisha
takribani kilo 2700 za dhahabu kwa mwaka ambapo pia umetoa ajira kwa
wafanyakazi 800, licha ya wale ambao wanafaidika kwa kuuza vyakula mgodini na
kadhalika.
Pamoja na kushiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Mang’onyi, lakini pia Kampuni ya Shanta
imeanzisha Mradi
wa maji kijiji cha Mangonyi (Kisima
kimoja kirefu kina meta 60, miundombinu ya kusambaza maji yenye urefu wa
kilomita 1.3, injini na pampu ya kusukuma maji kwenda kwenye tenki la kijiji na
polisi, imechangia Madawati 100,
sawia na Samani (yaani vifaa vya ofisi) ya Kijiji hicho.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu ameipongeza Kampuni ya Shanta kwa kutekeleza ahadi yao kwa wakati
kwa kuanza kuwalipa wananchi hao fedha zao za fidia kwa wamiliki wa mashamba
zaidi ya 130 ambapo zaidi ya watu 85 ndio watakaonufaika na kuifanya leseni ya kampuni hiyo itaanza
kufanya kazi.
Dc Mtaturu amesisitiza agizo lake alilolitoa la
kuitaka Kampuni hiyo kuwalipa fidia wananchi 69 wakati wa kikao cha pamoja
kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi
wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi ambacho
kilipewa jukumu la kuhakikisha wananchi wote ambao watapitiwa na mradi huo
wanalipwa fidia sambamba na kusimamia uhamishaji wa makazi.
No comments:
Post a Comment