Monday, September 19, 2016

TANGA SIMENTI WAZINDUA SIMENTI YA MWENDOKASI.

 Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kuitambulisha bidhaa mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano wa Tanga Simenti, Mtanga Noor
 Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Siment, Leslie  Massawe(Wapili kutoka Kulia) akiwa na wafanyakazi wa Tanga Simenti wakionesha mfuko wa Simenti wa Kilo 50 wakati wa uzinduzi na kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Tana Simenti wakiwa kwenye mkutano wa kuitambulisha Simenti mpya ya Mkombozi- simenti ya mwendokasi jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano wa Tanga Simenti, Mtanga Noor akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni  Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe.

TANGA CEMENT Public Limited Company (TCPLC) wazalishaji wa simenti hapa nchini wamezindua bidhaa bora ya simenti inayoitwa, MKOMBOZI.
 “Bidhaa hii mpya ya Tanga Cement ni hatua nyingine ya kuwa karibu na Watanzania kwa kubuni na kuwaletea aina nyingine ya simenti, ambayo mbali na kuwa ni ya bei ya kuridhisha kwa Mtanzania wa kawaida bado inawahakikishia ubora dhabiti unaoendana na teknolojia ya kiwango cha juu katika utengenezaji wa simenti”.

Ameyasema hayo wakati wa kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi, Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Siment, Leslie jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa mahitaji ya wananchi ni makubwa kukabiliana na ongezeko la miradi ya miundombinu na wakati huo huo mahitaji ya simenti bora katika ujenzi miundombinu na nyumba za makazi katika maeneo ya mijini na hasa vijijini ambapo utaalamu katika ujenzi.

Bidhaa mpya ya simenti ya MKOMBOZI – ‘simenti ya Mwendokasi' inaletwa kwa Watanzania ili kuharakisha maendeleo ya makazi bora na shughuli nyingine za ujenzi kama jina linavyojieleza.

MKOMBOZI, simenti ya daraja la nguvu kwa kiwango cha 32.5 N, ni simenti ambayo   bei yake ni ya kuridhisha ambapo mtu yeyote anayehitaji simenti kwa ujenzi wa aina yoyote anaweza kununua. 

Mkombozi imekuja kuwapatia watanzania kile wanachohitaji katika ujenzi wa miundombinu pamoja na makazi hii ni simenti kwa matumizi yote, simenti kwa aina zote za ujenzi.

No comments: