Monday, September 19, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI SPIKA MSTAAFU SAMUEL SITTA PIA ATEMBELEA KWA KUSHTUKIZA OFISI ZA MAGAZETI YA UHURU NA MZALENDO JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta anayeendelea kupata matibabu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mke wa Mzee Sitta, Mama Margaret Sitta. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta akiongoza Sala mara baada ya kujuliwa hali na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.kushoto ni Mke wa Mzee Sitta, Mama Margaret Sitta.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati akitoka katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakielekea kwenye Ofisi za Magazeti ya Uhuru na Mzalendo zilizopo katika mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wafanyakazi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Magazeti hayo zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wafanyakazi hao wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakwaza (kulia) pamoja na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti hayo Ramadhani Mkoma wakwanza (kushoto) wakiomba dua mara baada ya kumaliza kuzungumza na wafanyakazi hao jijini Dar es Salaam
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kushoto pamoja na Msemaji wa  CCM Christopher Ole Sendeka mara baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru wakaazi mbalimbali wa jijini Dar es Salaam waliokuwa wakimsubiri nje mara baada ya kuskia kuwa amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Magazeti ya Uhuru na Mzalendo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments: