Na Greyson Mwase
Serikali imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye
sekta za mafuta na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika
ukuaji wa uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya
Nishati na Madini Mhandisi Petro Marwa kwenye maonesho ya
kimataifa ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Petro alisema kumekuwepo na dhana kuwa wawekezaji
kutoka nje ya nchi wanapewa kipaumbele katika uwekezaji kwenye gesi
na mafuta jambo ambalo si sahihi.
Alisema ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na uwekezaji
kwenye sekta za gesi na mafuta, Serikali imeweka sheria nzuri za
kuwezesha watanzania kuwa sehemu ya uchumi wa gesi na mafuta.
“ Kwa mfano Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kifungu cha 218
kinaeleza ushiriki wa serikali kupitia Kampuni ya Mafuta ya Taifa
(National Oil Company) na kifungu cha 219 na 220 kinaainisha ushiriki
wa watanzania katika utoaji wa huduma na bidhaa kwa makampuni
yaliyowekeza nchini kwenye sekta za mafuta na gesi,” alisema
Mhandisi Petro.
Mhandisi Petro aliendelea kusema kuwa serikali imeweka mikakati
mbalimbali kuhakikisha watanzania wanakuwa si watazamaji kwenye
uvunaji wa rasilimali za gesi na mafuta bali wanakuwa ni washiriki kamili
na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akielezea mikakati hiyo, Mhandisi Petro alisema kuwa Serikali kupitia
Wizara ya Nishati na Madini ilianzisha kozi mbalimbali zinazohusu
mafuta na gesi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini (MRI).
Aliongeza kuwa Wizara imekuwa ikiwezesha wanafunzi wanaofanya
vizuri katika masomo ya sayansi kupata ufadhili wa kusomea masuala
ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mhandisi Petro alitoa wito kwa watanzania wote kuchangamkia fursa
zilizopo katika sekta za mafuta na gesi ili nchi iweze kutoka kwenye
kundi la nchi masikini duniani na kuingia katika orodha ya nchi zenye
kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa
inavyofafanua.
Afisa Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) kutoka Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu
yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo
kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo (kushoto)
akielezea majukumu ya Wizara kwa mteja aliyetembelea banda hilo
katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania
(TGDC) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa
ya Saba Saba (Dar es Salaam International Trade Fair)
yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba
Saba (Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika
picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es
Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Neema Mwambenja kutoka Taasisi ya Environmental Foundation for
Tanzania (EFFORT) ambayo ni mdau wa Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) (katikati) akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo
kwenye banda la REA, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Odriana
Magige kutoka taasisi hiyo.
Mhandisi Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Suleiman
Khalid (katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Kushoto ni Afisa Usalama na Mazingira kutoka shirika hilo Paul Thobias.
Banda la Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi zake kama
linavyoonekana pichani kwenye kwenye Maonesho ya Kimataifa ya
Saba Saba (Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea
katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini
Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza
kuwahudumia wateja katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment