Friday, July 1, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Baadhi ya wabunge wametoa maoni yao kuhusu mkutano wa bunge uliokua mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti. https://youtu.be/FwCAFpUGYgE

Baadhi ya wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya 40 ya biashara wameonesha wasiwasi WAO kutokana na kuwepo kwa wateja wachache kulinganisha na miaka mingine.https://youtu.be/GKD807LWqq0

Ikiwa ni siku ya mwisho ya kuhakikisha tatizo la madawati lina kwisha halmashauri ya wilaya ya Kasulu imetengeneza madawati 4500 kati ya 12000 yanayohitajika.https://youtu.be/NXErezYr5Ms

Jeshi la polisi nchini limesema muda wowote kuanzia sasa litaanza kuzisaka silaha ambazo hazijahakikiwa na wamiliki wake. https://youtu.be/dx6aJAIJP2A

Wadau wa sekta ya ardhi wameaswa kushirikiana na serikali ili kupatikana kwa hati za kutosha za wananchi za umiliki wa sehemu ya jengo. https://youtu.be/_NudxfBqxgM

Zaidi ya wakazi 6000 wa kata ya Igoma wilaya ya Mbeya wameanza kunufaika na huduma za afya baada ya mwenge wa uhuru kuzindua zahanati ya kijiji cha Kimondo.https://youtu.be/WtfjQNOkcrY

Kampuni nane za Kijerumani zinazoshiriki katika maonesho ya sabasaba zimesema zinahitaji ushirikiano wa kibiashara na kampuni za Tanzania.https://youtu.be/IXRoQqoOnyA

Wadau wa sekta ya utalii nchini wameiomba serikali kuondoa gharama za kodi ya ongezeko VAT kutokana na watalii kupungua. https://youtu.be/S4MSb922F34

Diwani wa kata ya Kigamboni jijini Dare s Salaam kwa kushirikia na wadau wa maendeleo wamejenga soko jipya la Kigamboni. https://youtu.be/uAycK2u_lTU

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na Doris Foundation wametoa msaada wa vyakula kwa wananchi wanaoishi kwenye mazingiara magumu Unguja.https://youtu.be/RMPKV9SSkcM

Benki ya Akiba Commercial bank ACB imetoa msaada wa shilingi milioni 12 kusaidia futari na daku kwa watoto yatima. https://youtu.be/2nYpW_T_o0s

Wahudumu wa baa na hoteli wametakiwa kuwa na ubunifu wa vyanzo vya mapato ili waweze kujikwamua kiuchumi. https://youtu.be/kwDktdlbBkg

Washiriki 25 wa mbio za magari wanatarajiwa kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa yatakayofanyika huko Bagamoyo. https://youtu.be/wjPgceGU6Fk

Timu ya African Lyion imeingia makubaliano ya kukuza vipaji vya michezo ikishirikiana na choise fm. https://youtu.be/gukPCFCAWM4

Shirikisho la soka nchini TFF limetanganza kuanza kusimamia michezo yote ya kimatifa inayofanyika hapa nchini. https://youtu.be/QvWEC_-GX0o

Michuano ya soka ya ligi ya wanawake kwa wilaya ya kinondoni inatarajiwa kuanza julai 10 kwenye uwanja wa Kifa Kinondoni. https://youtu.be/6xg7VEWbuh8

Tamasha la Eid El -Fitri litafanyika jijini Mwanza katika uwanja wa Nyamagana ambapo kutaendesha dua maalumu ya kuliombea taifa. https://youtu.be/AJ-myoRbH8g

Timu ya chuo kikuu cha Ekenford kilichopo mkoani Tanga imenyakua ubingwa wa mashindano ya vyuo vikuu nchini yaliyokua yakifanyika huko Dodoma.https://youtu.be/9r5eSlAl8C0

Spika wa baraza la wawakilishi mheshimiwa Zubery Alli Maulidi amesema kuanzishwa kwa bima ya afya kwa wajumbe wa baraza hilo ni hatua kubwa; https://youtu.be/e4j3yfjlMMg

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuboresha soko la Saateni ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa usalama zaidi ;https://youtu.be/gBsdxN6YM7k

Naibu katika katibu mkuu wizara ya Habari Zanzibar mheshimiwa Hassan Abdallah amewataka wakuu wa kitengo cha habari visiwani humo kutoa ushirikiano kwa viongozi wapya; https://youtu.be/ETZVaT0loCQ

Mamlaka ya anga Tanzania imekabidhiwa rasmi bawa la ndege lililookotwa visiwani humo kwa ajili ya uchunguzi zaidi; https://youtu.be/yQqT3z702EU

Idara mbalimbali za serikali zimeshauriwa kutoa elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar ili kuendelea kunufaika na utalii wa mji huo;https://youtu.be/5kTut0GlmIo

Tume ya Taifa ya uchaguzi visiwani Zanzibar imekabidhi ripoti ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka huu; https://youtu.be/5c8JN7LhYvw

Mkuu wa wilaya ya Kaskazini ndugu Hassan Alli Kombo amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidii pamoja na maadili ili kufikia malengo ya halmashauri hiyo; https://youtu.be/S3mIU8GrlK8

No comments: