Thursday, July 21, 2016

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ALLY SALUM APOKEA MSAADA WA MADAWATI 500 TOKA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

Mkuu wa Wilaya ya Kinondo jijini Dar es Salaam, Ally Salum(watatu kushoto) akikata utepe kuashiria kupokea kwa madawati 500 yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani.Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani jijini.Kutoka kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Janester Emily,Kaimu Afisa elimu shule za msingi kinondoni,Chitegese Dominic, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salam,Ally Salum akiwasisitiza jambo baadhi ya wanafunzi wa darasa la 4 wa shule ya msingi Mchangani iliyopo Mwananyamala Kisiwani jijini, wakati wa hafla ya kupokea msaada wa madawati 500 kwa ajili ya shule za 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ally Salum akimsalimia mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mchangani iliyopo Mwananyamala Kisiwani jijini, Hashim Jumanne baada ya kupokea msaada wa madawati 500 kwa niaba ya shule za 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondo jijini Dar es Salaam, Ally Salum akiongea na wanafunzi pamoja na Uongozi wa Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani, wakati wa hafla ya kupokea msaada wa madawati 500 yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule za 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani,Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam,wakiwa wamekalia madawati kati ya 500 yaliyotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani,wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati hayo jana.

2 comments:

Unknown said...

Mashaallah jamani naikumbuka shule yangu daah mwalimu mkuu emily bado yupo

Unknown said...

Mashaallah jamani naikumbuka shule yangu daah mwalimu mkuu emily bado yupo