Naibu balozi wa Ubalozi wa China Bw. Gou Haodong akizungumza katika uzinduzi wa duka la simu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora akiwa katika picha ya pamoja.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jijini Dar es Salaam.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora ameipongeza kampuni ya Huawei Tanzania katika juhudi zake endelevu za kuleta teknologia ya mawasiliano yenye kiwango cha juu kwa watanzania, kufuatia uzinduzi rasmi wa duka la 7 la bidhaa za Huawei na kitengo cha huduma kwa wateja katika duka la Mlimani City, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mapema mwaka huu Huawei Tanzania walianzisha mpango wao wa kuongeza mtandao wao wa usambazaji nchini kote kwa kuongeza maduka ya bidhaa zao nchini kote. Uzinduzi wa duka la bidhaa zake la Mlimani City ni mwitikio wa uhitaji unao ongezeka wa bidhaa za Huawei nchini na kuhakikisha kuwa bidhaa za Huawei na huduma zake zinapatikana kwa urahisi kwa wateja wa Tanzania.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu Huawei Tanzania imefanikiwa kuzindua maduka 7 ya bidhaa zake na kuongeza idadi ya mawakala wake nchini. Miongoni mwa maduka hayo ni duka liliolopo Mtaa wa Samora, City Mall na JM Mall jijini Dar es Salaam na maduka mengine mengi katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya.
Huawei Tanzania inatarajia matokeo mazuri katika duka lake la Mlimani City na kitengo cha huduma za simu kufuatia mauzo mazuri na huduma vilivyodhihirishwa na maduka mengine ya Huawei nchini kote. Duka hili la 7 la bidhaa za Huawei na kitengo cha huduma kwa wateja la Mlimani City ndilo kinara cha maduka yote ya Huawei Tanzania. Duka hili linawaahidi watanzania bidhaa na huduma za ubora wa juu kabisa.
Huawei imekuwa mstari wa mbele daima katika ubunifu na mabadiliko ya kiteknolojia kwa kwenda sambamba na mabadiliko na mahitaji ya wateja.
“Tumehakikisha kuwa tunakidhi kila mahitaji ya wateja wetu, hata hivyo tumeenda mbali zaidi kwa kuzingatia tofauti za vipato vyao na matumizi kwa kuwaletea bidhaa ambazo zitakidhi haja ya kila mteja wetu”. Alidhihirisha Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Levin Zhang (Yongquan), katika hotuba yake ya sherehe ya ufunguzi.
“Huawei Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa nchini na imejikita katika kuhakikisha ukuaji na maendeleo ya sekta ya mawasiliano nchini. Tangu kuanzishwa kwa shughuri zetu nchini, tumeshirikiana na sekta mbalimbali ikiwamo serikali katika kuipeleka mbele TEHAMA. Huawei Tanzania imedhamiria kuwa kinara wa simu za kisasa Tanzania, kwa kuwapatia wateja wake simu bora na zinazotumika kwa urahisi.” Alidhihirisha mkurugenzi huyo.
Akiwahutubia wananchi wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi aliipongeza kampuni ya Huawei Tanzania kwa hatua waliyoichukua ya kuinua sekta ya TEHAMA nchini. Katibu mkuu huyo amepongeza juhudi zilizofanywa na Huawei Tanzania si tu katika kuleta mawasiliano bora na teknolojia kwa kupitia bidhaa zao nyingi za simu za kisasa bali pia kwa kuwezesha upatikanaji wa fursa za ajira kwa watanzania.
“Kwa miaka mingi sasa serikali ya Tanzania imekuwa na uhusiano mkubwa na Huawei Tanzania, na tumeshirikiana na kampuni hii katika miradi mingi kwa mafanikio makubwa. Kwa kupitia ubunifu wao katika eneo la TEHAMA, Huawei imeendelea kuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu. Ufunguzi wa duka hili hapa Mlimani City ni hatua ya mwendelezo wa juhudi zake kwa wateja wake wa Tanzania ambao wanauhitaji mkubwa wa teknolojia ya mawasiliano.
Nina matumaini kuwa kwa kupitia hatua mabalimbali ambazo serikali imechukua katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili TEHAMA na kwa mwendelezo wa ushirikiano wa wadau binafsi kama Huawei Tanzania, malengo yetu ya Milenia ya kuwawezesha watanzania kwa kupitia TEHAMA yatafikiwa”. Alisema Katibu Huyo.
Naibu balozi wa Ubalozi wa China Bw. Gou Haodong ambaye alishiriki sherehe za uzinduzi ameipongeza Huawei Tanzania kwa hatua yake muhimu ya kuboresha sekta ya mawasiliano ya simu nchini.
“Nina matumaini kuwa kampuni hii kubwa kutoka China itaendelea kuwekeza katika sekta ya mwasiliano hapa Tanzania. Naamini, kwa juhudi za pamoja baina ya serikali na Huawei zitaifanikisha Tanzania kuifikisha sekta hii katika viwango vya juu”. Alisema
Serikali ya Tanzania inatambua mchango wa Huawei katika kuhakikisha upatikanaji wa simu halisi hapa nchini. Kampuni hii pia imeendesha miradi kadha wa kadha ya kuendeleza vipaji vya TEHAMA nchini ambayo imewajengea uzoefu wnafunzi wa kitanzania na kuwaandaa kufanya kazi katika makampuni ya simu. Huawei pia imeteuliwa kuwa mshauri wa serikali wa TEHAMA, mradi ambao utaipa nafasi Huawei ya kutoa mafunzo ya TEHAMA, elimu na huduma kubwa za data.
Katika kusherehekea uzinduzi huu wa duka la bidhaa za Huawei Mlimani City, Huawei Tanzania inatoa punguzo maalum kwa aina kadhaa za simu kuanzia Julai 16 hadi 31. Huawei pia imetangaza uwepo wa tolea lake jipya kabisa lenye teknolojia ya juu zaidi la Huawei P9 katika soko la Tanzania. P9 ni simu ya kwanza duniani yenye kamera mbili, inayounda picha zenye kiwango cha juu kabisa. Kila bidhaa ya Huawei imekuwa ikibadili ubora katika ulimwengu wa simu katika hadhi na utendaji wake. Huawei P9 imeundwa kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya upigaji wa picha kwa simu katika viwango vipya.
No comments:
Post a Comment