Tuesday, July 5, 2016

Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Nyabaganga Taraba akabidhiwa ofisi

  
 Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilayani humo leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi. Katika hafla hiyo, Taraba aliwataka watendaji wa wilaya hiyo kujituma kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano pamoja na kuwa waadilifu katika kuwatumika wananchi.
Aidha, alimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo aliyestaafu, Hawa Ngh’umbi kwa utendaji wake huku akiahidi kuendelea kuchota hekima zake.

Mkuu wa Wilaya mstaafu, Hawa Ngh’umbi akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo wakati akiagwa baada ya kustaafu.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Wengine kuanzia kushoto waliokaa ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kangese, Mkuu wa wilaya mstaafu, Hawa Ngh’umbi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Wilson Nyamunda.

 Mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake, Hawa Ngh’umbi (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mkuu mrithi wake, Nyabaganga Taraba wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
 Mkuu mpya wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba akisaini nyaraka za makabidhiano ya Ofisi tayari kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo. Picha na Robert Hokororo  WA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU

No comments: