Tuesday, July 5, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Ujenzi wa barabara inayounganisha nchi za afrika mashariki umeelezwa kucheleweshwa na ujenzi wa madaraja makubwa na uhamishaji wa mabomba ya maji katika barabara hiyo. https://youtu.be/7TvPEEr96WI

SIMU.TV: Uwepo wa njia nyingi za panya katika maeneo ya Holili na Tarakea wilayani Rombo umesababisha kuikosesha serikali mapato. https://youtu.be/vuEx-PrGXyM

SIMU.TV: Sheikh mkuu wa Tanzania amesema kuwa mwezi umeandama na kuonekana maeneo mengi ya nchi hivyo kesho itakua ni sikukuu ya Eid Al Fitr.https://youtu.be/APExiHipBzU

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda ya maalumu ya Dar es Salaam limetoa tahadhari kwa wakazi wa Dar es Salaam kujiepusha na vitendo vya kihalifu katika msimu huu wa sikukuu.https://youtu.be/A7fpjtwN6is

SIMU.TV: Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ally Mohamed Shein ametoa wito kwa watanzania kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ili kuinua soko la bidhaa hizo. https://youtu.be/sIBm6kSPugA

SIMU.TV: Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza limetoa utafiti wake kuhusu masuala ya muungano wa Tanzania ambapo asilimia 42 ya watanzania pamoja na mambo mengine wanasema rais wa Zanzibar akubalike na kutambulika kama rais.https://youtu.be/wrDzYr4Rk7k

SIMU.TV: Kampuni hodhi ya miundombinu ya reli imeanza kuwaondoa watu waliojenga na wanaofanya bisahara kando ya miundo mbinu ya reli. https://youtu.be/OS7ZaNiNAqc

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini imeeleza kuvuka lengo la kukusanya mapato kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016. https://youtu.be/vxJJ1oRwOiA

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano amewataka wanazuoni wa Tanzania kujifunza kutoka kwa wataalamu wa China ili kuwezesha kufikia nchi ya viwanda.https://youtu.be/jAp7N7MQ6OQ

SIMU.TV: Idadi ya mikopo iliyotolewa na benki ya watu wa Zanzibar PBZ mwaka 2015 imeelezwa kuongezeka ukilinganisha na ile iliotolewa mwaka 2014.https://youtu.be/4p9J82LA2Hw

SIMU.TV: Naibu waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo amekabidhi bendera ya taifa kwa timu ya wanawake kutoka Nachingwea mkoani Lindi kwenda nchini Finland kwa mashindano ya kombe la HELSINKI. https://youtu.be/9BU13qD2zAg

SIMU.TV: Vikundi mbalimbali vya watoto yatima vimepokea msaada wa vyakula kutoka kwa waandaji wa tamasha la pasaka kwa ajili ya sikukuu ya Eid.https://youtu.be/TeZIFq_AXag

SIMU.TV: Msanii Mrisho Mpoto pamoja na bendi yake wametoa burudani katika viwanja vya sabasaba wakihamasisha watanzania kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF.https://youtu.be/_QQtUQNw5g4

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela ameahidi kushirikiana na wadau wa soka wilayani humo ili kuinua mchezo wa soka. https://youtu.be/pXrGFsmdleo

SIMU.TV: Kesho timu ya Ureno itashuka dimbani kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya timu ya Wales katika michuano ya EURO. https://youtu.be/nu8vm-3I-gc

SIMU.TV: Mamlaka ya udhibiti usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA imesimamisha leseni za mabasi 12 ya kampuni City Boy kupisha uchunguzi zaidi;https://youtu.be/Vv_WkvEkEec

SIMU.TV: Kampuni ya AMGL inayomiliki kituo cha Channel Ten na Magic Fm radio leo kimekabidhi msaada wa chakula na vifaa mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Umrah; https://youtu.be/P7j-O_IBo4k

SIMU.TV: Kesho ni sikukuu ya Eid El Fitri ambapo waislamu nchini wataungana na waislamu duniani kote kusherehekea sikukuu hiyo baada ya kumaliza mfungo wa mwezi ramadhani; https://youtu.be/uIQLIwYGYjE

SIMU.TV: Serikali imesema imejidhatiti katika kulinda mipaka yote ya nchi na kuwachukulia hatua wale wote watakaohusika katika kusafirisha wahamiaji haramu;https://youtu.be/KvorYcUeFI0

SIMU.TV: Kampuni ya simu za mkononi Vodacom imezindua ofa maalumu kwa wateja wake itakayowawezesha kutuma meseji na kupiga simu kadri watakavyo;https://youtu.be/dFwAM-2g13E

SIMU.TV: Ofisi ya rais menejiment ya utumishi wa Umma  imetangaza makatibu tawala wa wilaya wapya ili kuziba nafasi za waliofariki, wazee na wengine kupisha wenzao wateule;https://youtu.be/fxRa2vQyNBY

SIMU.TV: Dhamira ya kweli ya kubadilika kifikra na mitazamo ndio nguzo pekee ya kufikia lengo la nchi kufikia Tanzania ya viwanda; https://youtu.be/f51f8zI0CoU

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini TRA imevuka lengo la ukusanyaji kodi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 baada ya kufanikiwa kukusanya trilioni 13 na kuvuka lengo walilopangiwa na serikali; https://youtu.be/bp3iuaZBPpI

SIMU.TV: Tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar ZIFF linatarajia kuanza Julai 9 visiwani humo huku wageni mbalimbali maarufu wa kimataifa wakitarajia kushiriki;https://youtu.be/pzF1Y8enMfA

SIMU.TV: Naibu waziri wa habari utamadani na michezo Anastazia Wambura, amekabidhi bendera kwa timu ya Taifa vijana ya wanawake wanaokwenda nchini Finland kushiriki michezo mbalimbali nchini humo; https://youtu.be/w4ypK6_2Bh4
SIMU.TV: Kampuni ya Msama Promotion imetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwa watoto wenye uhitaji huku wakiwataka wananchi kujitolea chochote walichonacho kwa watu wenye uhitaji; https://youtu.be/ktRVN2cAkYY

SIMU.TV: Msanii wa muziki nchini Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amewaasa wasanii kuweka akiba ya baadae ili kukwepa kudhalilika na kujiingiza katika anasa ziizo za lazima; https://youtu.be/oKJ8HPYDHHE

SIMU.TV: Kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho amesema anasikia faraja kuwa katika timu ambayo alikuwa anatamani kuwepo kwa muda mrefu huku akiahidi kushinda mataji lukuki akiwa hapo; https://youtu.be/er86pXlB2tc

No comments: