Tuesday, July 5, 2016

Rais Dkt. Shein atembelea maonesho ya Sabasaba Dar es salaam

 Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiliamali  wanawake wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mke wa Rais wa awamu ya tatu Mama Anna Mkapa.
 Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein  akipata maelezo toka kwa mjasiliamali juu ya vyakula vilivyosindikwa wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere.

 : Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akiangalia mafuta ya kula yanayotengenezwa na wajasiliamali , wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
 Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiuliza swali kwa mjasiliamali wakati alipotembelea banda la wanawake Wajasiliamali  (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. 
 Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Waziri  wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Balozi  Amina Salum Ali,wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.               
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko zanzibar Balozi Amina Salum Ali(wa tatu kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) wakati alipotembelea leo katika maonesho ya 39 yaa Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia biashara mbali mbali za vipodozi wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  Balozi Amina Salum Ali na kulia mjasiria mali Fadhil Mohamed wa Kiembesamaki Zanziba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia biashara mbali mbali za vipodozi wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiangalia biashara mbali mbali za viatu vya Makubadhi na Mikoba  wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar, leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipangalia mashine ya kutengenea sabuni pamoja kuapata melezo kutoka kwa Mkurugenzi George M.Buchafwe  wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam leo (kulia) mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Ziwanda vidogo vidogo (SIDO) Bw.Omar Jumanne Bakari
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Mkombozi Group (NGARABUTO) Bw.Amos Z.Mshina,kuhusu Usindikaji  na Usambazaji wa Unga wa Muhugo katika maeneo ya Sengerema Mkoani Mwanza,wakati  alipotembelea mabanda ya maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa leo yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia biashara mbali mbali ya mikoba  wakati alipotembelea leo  maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam,(kulia) Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOTF) Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa. Picha na Ikulu.

No comments: