Sunday, July 10, 2016

KAMPUNI YA MANTRA YAMWAGA MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI WILAYANI SONGEA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilnith Mahenge (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Frederick Kibodya alipofika katika kata ya Majengo kupokea msaada wa madawati 500 yaliyotolewa na kampuni hiyo.
Mtendaji kata ya Majengo katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Yusuf Mshamu (kulia) akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilnith Mahenge aliyetembelea katika kata hiyo kupokea msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 40 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo.
Sehemu ya madawati 500 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania yakiwa tayari kabla ya kukabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge yatakayosambazwa katika shule za msingi wilayani Songea kwa ajili ya kukabilianana upungufu wa madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge wa kwanza mbele akikagua sehemu ya madawati 500 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo mkoani humo,katikati nni mkuu wa wilaya ya Songea Oraleti Komando Mgema na wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Mantra Frederick Kibodya.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mantra inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo, Frederick Kibodya (kushoto), akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge moja kati ya madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 40 ili yasaidie kupunguza tatizo la madawati kwa shule za msingi mkoani Ruvuma.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Bilinith Mahenge akikabidhi moja ya madawati 500 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, Oraleti Komando Mgema ili yasaidie kupunguza uhaba wamadawati kwa shule za msingi wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Bilinith Mahenge akizungumza na wananchi,viongozi na wawakilishi wa kampuni ya Mantra Tanzania katika viwanja vya stendi ya malori kata ya Majengo katika manispaa ya Songea baada ya kupokea msaada wa madawati 500 kutoka kwa kampuni ya Mantra inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo.

No comments: